Jumanne, 31 Januari 2017

THE POWER OF LOVE SEHEMU YA 08

HADITHI.
THE POWER OF LOVE.
SEHEMU YA 08.
Picha ya Hamis Mpendu Jr.
ILIPOISHIA JANA
"Taap" issa aliudaka mkono wa zarina kisha akatengeneza ngumi ya haja hapo akakusanya nguvu kisha akaishusha ngumi ile kunako pua ya zarina,,
"Mama weeeeeee"
TAMBAA NAYO SASA
Zarina alipiga ukelele huku akiwa amefumba macho ya kwa woga hata kabla hajafikiwa na ngumi tayari jasho la majuto lilianza kumtawala hapo akajikuta anapiga ukelele wa hofu,, issa alipeleka ngumi lakini hata hakuwa ameifikisha alipo kusudia mkono wake ulikuwa umeganda karibu kabisa na uso wa zarina,,
"Sina haja ya kukupiga japo uwezo wa kufanya hivyo ninao,ushukuru sana moyo wangu uliotowa msamaha kutokana na upendo juu yako,umasikin wangu bado hujawa kikwazo cha kusitisha hisia zangu kwako amini nakupenda sana zarina,,
"Huuu" issa alishusha pumzi kisha akaendelea na siasa zake,,wakati huo zarina alisha yafumbu macho yake na alikuwa mpole kama sio yeye,,
"Moyo wangu unakuwaza wewe badala ya kusukuma damu,naomba usinichukie kutokana na umasikini wangu tambuwa aliyekupa wewe kwenye kikapu ndye aliye nipa mm kwenye kijiko" ,,issa aliongea huku akitokwa na machozi haikuwa kazi rahisi kwa mtu mwenye utimamu wa akili kuyafanya yale akiwa amezungukwa na mashila wadu wa kila aina,,
"Popote uendapo katika hii dunia tambuwa kuna mtu mmoja anakupenda sana na simwinge ni mimi issa" baada ya maneo hayo hakuwa na sababu ya kuwa pale hapo akauwachia mkono wa zarina kisha akaanza kupiga hatuwa kwa mwendo wa kiminyato,,
Zarina alitamani kulitaja jina la issa lakini alihisi kama amebanwa na kitu kizito kunako koo lake hapo akaliendea gari lake hata alipofika alitumbukia ndani kisha akakilaza kichwa chake kunako usukani kazi yake ikawa ni kumwaga machozi huku kamasi nyepesi zikiendelea kusurubu pua zake, alitamani ashuke angalau akaupate msamaha wa issa lakini alivyotaka kunyanyuwa mguu alijikuta anashindwa hata asijuwe hali hiyo inatokana na nini,,hakuwa najinsi tena hapo akawasha gari lake na kutimuwa zake,,
"Mwanangu we boya kinyama,yani unapigwa na demu daah, ingekuwa mm saizi tushagawana majengo ya serikali" maneno hayo yalimtoka jamaa mmoja aliyeitwa dossa, suluali yake ilikuwa chini ya makalio huku akiwa kashika sigara kubwa, moshi aliutolea puani na kujiona yeye ndo yeye,,
"Poa nkaushie basi"
" sio nkukaushie umezingua sana Bob"
"Achana na mm bac, mm siwezi kumpiga demu coz sio domo zege kama wewe",,,kauli hiyo alikuwa kama mwiba kwa dossa ukweli hata yeye alimpenda sana zarina ila alishindwa kumwambi, kitendo cha kumuona issa katema voko kilimuuma sana na kwajinsi alivyopangilia maneno yake alikuwa na asilimia zaidi ya mia kumpata zarina,,dossa alivyo lijuwa hilo alitaka kuulidhisha moyo wake kwa kumfanyia shari jerani yake kwa biashara,,
" nani domo zege ee, nakuuliza wewe"
"Paaaah'" dossa aliongea kwa jazba kisha kikamtoka na kibao,,
Issa hakuwa na haja ya kuonekana mjinga kwa mara ya pili hapo bila ya kuchelewa akamvamia dossa na varangati likaanza,licha ya upole wake issa lakini alibarikiwa ubavu wa maana hata hakuchukuwa dakika nyingi tayari dossa alikuwa chini huku damu zikiendelea kumtoka mdomoni achilia mbali uvumbe uliojitokeza kunako uso wake,,akiwa chini dossa aliwaza na kuwazua kitendo cha kutolewa damu aliona ni ujinga uliopitiliza hapo akazama kunako mfuko wa suluali yake kisha akatoka na bisi bisi moja yenye ncha kali,kwa kasi ya umeme dossa aliruka kama nyoka na kuikandamiza bisi bisi yake kunako bega la issa,,
"Mtumeee" baadhi ya mashuhuda walijikuta wameduwaa hamu yao ya kutazama ungomvi iliwatokea puani,kilicho waogopesha zaidi ni zile damu zilizo kuwa zinatiririka mithiri ya maji ya bomba,,
Wakati huo dossa alikuwa anamaliza chochoro za mitaa ya buguruni hakuwa na sababu ya kubaki eneo lile tena alichangana miguu yake na kutokomea alipo pajuwa mwenyewe,, wale walio yafurahisha macho yao hivi sasa walikuwa na jukumu la kumkusanya issa aliyekuwa anagagaa kwa maumivu na kumuaisha hospital,,
*****************
Usiku wa siku hiyo hakuupata usingizi kazi yake ilikuwa kupapasa foronya za mito alitamani masaa yarudi nyuma ili auzuie mdomo wake kwa maneno machafu au masaa yasonge kwa haraka ili akaupate msamaha wa issa lakini haikuwa ivyo,aliendelea kuwaza huku akitokwa na machozi ya majuto,,
"Popote uwendapo katika hii dunia tambuwa kuna mtu mmoja anakupenda sana na simwingine ni mimi issa" maneno hayo yaliendelea kuumiza mtima wake, hatimaye usingizi ukamzidi nguvu,
Siku iliyofata alifanya mambo yake kwa haraka hata alipo maliza alijikusanya na kuelekea sokoni,,bahati haikuwa upande wake kwani aliye msumbukia hakuweza kumkuta hapo akajalibu kusubili na kusubili lakini wapi ,,alitamani kuuliza lakini aliiogopa jeuri yake aliyoionyesha jana mbele ya kadamnasi ya watu,,hapo akaamuwa kutimka zake,,siku ya pili hali ilikuwa ni ile ile tu hata siku ya tatu bado hakuweza kuishuhudia sura ya issa, hatimaye wiki ikatokomea lakini issa hakuonekana,,
Kutokana na mawazo juu ya issa ilimfanya apoteze hamu ya kula, mwili wake ulidhohofika kupita maelezo,,sio siri zarina aligeuka mtumwa wa mawazo, siku moja alipanga kwenda hospital angalau kucheki afya yake kwa maana alizidi kuteketea siku baada ya siku,,alifanya taratibu zake hata alipozimaliza alikuwa njiani kuelekea hospital, hakutaka kupita njia ya rami hapo aliongoza barabara ya vumbi kuelekea bungoni akiwa na nia ya kuiendea hospital la amana,, hata alipofika alishuka kunako gari lake na kupiga hatuwa kuliendea jengo la hospital,, akiwa mlangoni almanusura apige kelele kwa maana alicho kiona kilimuogopesha sana,,
"Issaaaa!!!" Zarina aliropoka hivyo akiwa kwenye mshangao,,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni