Jumanne, 31 Januari 2017

KENGERE YA KIFO SEHEMU YA TATU(03).



Riwaya: KENGERE YA KIFO
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CONTACT: 0656292416
Picha ya Yozz Piano Maya Tz
SEHEMU YA TATU(03)
***ilipoishia***
Mzee Sule aliliendesha gari mpaka kule porini ilipokuwepo nyumba yake...alipofika alishuka kutoka ndani ya gari kisha akalivuta furushi lile na kuliweka begani
akazioiga hatua kuingia ndani ya nyumba yake...akapitiliza mpaka ndani ya chumba kilichokuwa kimejitenga peke yake...akalitupia juu ya meza lile furushi...akachukua kusu pamoja na shoka na Upanga mkali sana....akachana furushi lile na kutoa lile turubai alilokuwa amelifunga...alipo litoa turubai hilo,,ndani yake ilikuwemo maiti ya yule rafiki yake Domy......Sule akachukua shoka na kuanza kuikata kata maiti ile..na kukata nyama isiyokuwa na mifupa na kuiweka ndani ya ndoo.....
***Endelea***
akakata viganja na miguu na kuviweka kwenye mashine ya kusagia nyama unayotumia umeme...mzee sule alikuwa na mtambo maalumu unaofua umeme kwa kuakisi mionzi ya jua.mashine hiyo ilikuwa na nguvu..inauwezo wa kusaga mpaka mifupa ikawa unga mlaini kabisa...
viganja pamoja na miguu iliyosagwa aliitumia kutengenezea soseji pamoja na sambusa.....
alipomaliza kukata kata nyama hiyo alichukua shoka akakipasua kichwa na kutoa ubongo akauweka pembeni vilipokuwepo utumbo pamoja na maini na figo....ambavyo huvichanganya kwenye supu matata...
alipomaliza alichukua ndoo iliyojaa maji na kiisafisha meza kwa kufuta damu zilizomwagika....kisha akabeba ile ndoo iliyokuwa imejaa nyama pamoja na ndoo nyingine iliyokuwa na utumbo pamoja na maini,,figo na ubongo...akazipiga hatua kuelekea kwenye chumba chake cha kulala aka vuta kochi kulisogeza kando...akafungua mlango mdogo uliokuwa kwenye sakafu..mlango huo ulitengenezwa kwa mbao ngumu...... akaingia uoande wa ndani kisha akazichukua ndoo hizo mbili akaanza kuzioiga hatua kwa kupitia nja hiyo ya chini kwa chini kuelekea kuke kwenye mgahawa...
*****************
upande mwingine alionekana Domy akiingia nyumbani kwake....Tina alimpokea mumewe wakazipiga hatua kuelekea chumbani..walipoingia Domy alisema anahisi uchovu..hivyo anahitaji kupumzika.....akapanda kitandani akajipumzisha
Tina akatoka na kuelekea jikoni.....akaandaa chakula cha jioni...
*****************
upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee sule ilisikika sauti ikisema,,""Niongezee supu nalafu ongeza sambusa mbili....
wakati huohuo alionekana mzee sule akitokezea jikoni kutoka kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini ya aridhi....mke wake alichuku ile ndoo iliyokuwa na nyama akaiweka kwenye sufulia kubwa akaweka maji na kuliweka juu ya jiko....
kisha akachukua sufulia lingine akaanza kuosha utumbo kisha akaubandika jikoni huku akisema,," mme wangu leo umechelewa yani supu ilikuwa imekaribia kuisha alafu leo wateja ni wengi sana si unajua ni weekend(siku ya mapumziko)
*****************
Upande mwingine alionekana muuza maziwa akiwa amebeba mitungi iliyokuwa na maziwa ndani yake....mitungi hiyo iliyotengenezwa kwa bati la aluminiamu...alikuwa kaifunga vyema kwenye kiti cha nyuma........huku akiendesha baiskeli.....akapiga kengere huku akipaza sauti,,"MAZIWA MAZIWA MAZIWA....mtu huyo hakuwa mbali na nyumbani kwa Tina..
wakati huo huo Domy alionekana akinyanyuka kitandani ili akamwambie tina kuwa yeye anajisikia kula mboga kavu isiyokuwa na mchuzi..
Wakati huo huo Tina alionekana akiendelea kuandaa chakula..ghafla akastuka baada ya kusikia sauti ya kengere akaanza kubadilika,,macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu......ghafla kisu alichokuwa amekishikilia mkononi kikadondoka chini kutoka mkononi.....akanyanyuka na kusimama wima akazipiga hatua za taratibu ghafla akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya yule muuza maziwa....
yule muuza maziwa akastuka akashika breki ya ghafla baiskeli ikaserereka na kuanguka chini....Tina akamkamata na kunyinga kwa kutumia kamba yake....kisha akatoweka kimiujiza.....akajitokeza nyumbani kwake.....baada ya sekunde kadhaa akarudi katika hali yake ya kawaida...akawa anajishangaa ghafla Domy aliingia jikoni akamkuta Tina kasimama huku anaonekana kuushangaa mwili wake..
Domy akauliza,,,"umepatwa na nini mbona unainekana kujitazama mwili wako????
Tina hakujibu kitu alibaki kimya...ghafla fahamu zikarudi akastuka sana nusu akimbie....
***************
upande mwingine kule aliponyongwa muuza maziwa......kwa mbali lilionekana gari la Mzee sule likiishirizi kwenye kona huku limebeba baiskeli upande wa nyuma ya gari.....
Kule nyumbani kwa Domy....Tina aliamua kumdanganya Domy kuwa kichwa kinamuuma..huku akijishika usoni..Domy aliogopa akaamua ampeleke hospitali haraka..akamchukua Tina huku ameuweka mkono wa Tina Begani kwake wakazipiga hatua kuelekea kwenye gari ili waende hospitali....Domy aliliwasha gari na kuliondosha kwa kasi.
wakiwa njiani karibia kwenye mataa...walikuta foleni ikawalazimu wasubiri foleni...
pembeni kulikuwa na gari jingine limesimama..ndani ya gari hilo kulikuwa na familia alikuwemo Mwanamke Mtoto pamoja na baba wa mtoto ambaye aliyekuwa akiliendesha gari hilo....kulikuwa na vitu vingi vya kuchezea mtoto wao ndani ua gari hilo ghafla yule mtoto akachukua kengere ya kuchezea watoto.......mtoto hiyo aliitingisha kengere ile kwa kuigonga gonga kwenye kiti cha gari....ghafla Tina akasikia mlio wa kengere hiyo.....akastuka.
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya nne(04)
pia usisahau ku-Like page yangu inayoitwa
MAYA WA HADITHI .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
like pia share na marafiki.
ASANTENI...

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni