Ijumaa, 20 Januari 2017

SIMULIZI YA PETE YA AJABU..KUANZIA SEHEMU YA1-7

HUU NI MUENDELEZO WA SIMULIZI YA PETE YA AJABU..KUANZIA SEHEMU YA1-7 ISOME HAPA
KWA AMBAO HAMKUISOMA RIWAYA HII                                                                                                  
MAYA WA HADITHI🔴:
Riwaya: PETE YA AJABU
Mtunzi: Yozz Piano Maya
whatsapp 0656292416
Sehemu ya kwanza(1)
haiwezekani lazima iwe kwa namna yoyote ile labda sio mimi CHOTA nilijipa imani nikasema Maisha ni popote. nilijiseme kimoyomoyo" wakati huo nikiwa natembea taratibu kwa mwendo wa kujivutavuta kutokana na uchovu niliokuwanao" niliendelea kutembea huku nikikumbuka kwa kile nilicho kifanya jana usiku kule Studio....niliamini kuwa wimbo wangu utakuwa mzuri sana pale prodyuza (prodicer) wangu akimaliza kufanya mixing ya wimbo wangu ambao niliupa jina la ( USIENDE)" nilitabasamu na kisha nikajisachi (nikajipapasa mifukoni mwangu) hapo ndipo nilipogundua nilikuwa nimesahau Simu yangu studio pale chini ya meza.nilisita kutembea nilisimama kwa sekunde kadhaa huku nikijiuliza kutoka hapa nilipo mpaka kurudi studio ni umbali kama kilometa tono hivi! dah niliishiwa nguvu.. nikakumbuka pale nyumbani ninapoishi sio kwetu wala si kwa ndugu yangu; ni kwa rafiki yangu kipenzi na sikuwa na ufunguo kutokana na mlango huo ulikuwa unafunguo moja tu! aaaaah je nisipomkuta alafu namba zake zimo ndani ya simu yangu! nilijiuliza" lakini niliamua kurudi kuifuata simu yangu wakati nipo njiani nikielekea studio kwa lengo la kuifata simu yangu nilijihisi mwenye kuchoka sana" nilisita kutembea nikasimama nikalitoa(lasket) begi langu dogo nililokuwa nimelibeba mgongoni kwa nia ya kuchukua chupa ndogo ya maji niliyo nunua jana usiku" nilinyong'onyea baada ya kufungua zipu ya begi langu hilo dogo...sidhani kama yatakata kiu changu nilijisemea moyoni..kwani maji yaliyokuwa yamebaki ni kidogo sana hata nusu ya kikombe hayawezi kuenea.. nilisogea pembeni mwa barabara nikavuka mfereji nikaa pembeni ya duka moja ambalo lilikuwa linahusika na uuzaji wa vyombo vya ndani mara ghafla nikasikia sauti ikiita jina langu ikitokea upande wa pili wa barabara nilishtuka sana na mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda mbio kwa kasi ya ajabu nilijawa na uwoga wa hali ya juu baada ya kumuona............
Itaendelea......
je? ni nini/ ni nani aliemuona mpaka ikampelekea CHOTA kushtuka na kuingiwa uwoga? ungana na Yozz Piano Maya katika muendelezo wa PETE YA AJABU sehemu ya pili
MAYA WA HADITHI🔴:
riwaya:PETE YA AJABU
mtunzi:Yozz piano Maya
whatsapp 0656292416
Sehemu ya pili(2)
woga ulitawala ndani ya mwili wangu baada ya kumuona Mussa" musa alikuwa akinidai pesa zake elfu ishirini (20)ambazo alinikopesha miezi miwili iliyopota.
kwasababu aliniahidi kuwa popote atakapokutana na mimi endapo nisipomlipa pesa yake angenifanyia fujo angechukua chochote nilichonacho...alivuka mfereji na kuelekea upande niliokuwepo" habari za masiku (mingi)aliongea kiswahili cha mtaani na maneno mengine ya kejeri aaaah naona mambo yako super umeshine kinoma alisema Mussa" sikumjibu chochote niliendelea kukaa kimya huku nikitafakari nimdanganye nini ili a nielewe...lakini wakati huo nikiwa katika fikra za kumdanganya kuhusu pesa yake aliyokuwa akinidai" hapo nikakumvuka sauti ya marehemu baba yangu alishawahi kuniambi "sikuzote msema kweli ni mpenzi wa Mungu pia ukweli humuweka mtu huru" kabla sijaongea kitu chochote ilisikika sauti ya Mussa ikisema oya" vipi kuhusu pesa yangu? aliuliza Mussa..."
nilimjibu huku niking'ata maneno kama mtu mwenye kigugumizi daah" ndugu yangu naomba univumilie kwa sasa ninakipindi kigumu sana Musa alinipokonya begi langu dogo nililokuwa nimebeba mgongoni na kusema kwahasira maneno ambayo yalinifanya machozi kunyemelea kwenye macho yangu..kumbe wakati Mussa akifanya kitendo kile"
yule muuza vyombo aliona tukio zima na alikuwa akisikiliza kwa makini mazungumzo yetu..alitoka nje ya duka lake na kumsihi Mussa anirudishie (lasket) begi langu dogo lakini Mussa alikataa kata kata na akasema na bado sikunyingine nikikutana na wewe kama hautokuwa na pesa yangu nitachukua chochote ulichonacho"
nilikuwa Mnyonge sana nikashusha pumzi ya uwoga kisha nikamwambia Mussa nitakupatia pesa yako jumamosi inayokuja naomba unirudishie begi langu.
Mussa alinijibu kwa kejeri" unapenda vya bure eee utashikishwa ukuta (yani kugeuzwa kinyume na maumbile) kulikuwa na watu wawili wakipita pembeni yetu walicheka kisha wakaendelea na safari yao sikuweza kuvumilia kusikia kashfa hiyo . sikuwahi kufanya ugomvi wa aina yoyote tangu nilipotoka tumboni kwa mama yangu" nilikumbuka mambo mengi pia nilimkumbuka marehemu baba yangu '
laiti kama ungekuwa hai nisingedalilika hivi! nilijisemea moyoni" Mussa aliendelea kutoa maneno ya kejeri Mwanamuziki gani hauna hata elfu ishirini ya kulipa pesa ninayokudai?
ghafla nilijawa na gadhabu sikuwahi kuwa na hasira kiasi hicho nilijikuta nimempiga ngumi iliyotoka mkono wa kulia na kumpata baraabara kwenye jicho' nikarusha teke lililompata tumboni..teke lile lilimpelekea kuanguka ndani ya ule mfereji uliokuwa pembeni na pale tulipokuwa tumesimama
aliangukia kisogo na kujigonga kwenye kuta za pembeni mwa mfereji huo Mussa alitulia kimya huku damu nyingi zikimtoka kichwani kutoka na mpasuko baada ya kujigonga kwenye ukuta ule wa mfereji
Itaendelea................
[1/13, 21:01] MAYA WA HADITHI🔴: Riwaya: PETE YA AJABU
Mtunzi: Yozz Piano Maya
whatsapp 0656292416
Sehemu ya tatu(3)
niliogopa sana niliokota begi langu lililo dondoka chini kutoka kwenye mikono ya Mussa baada ya kumpiga ngumi ya jicho.. nikakimbia kwa spidi (speed) kutoweka eneo la tukio na kutokomea kusikojulika..nilikimbia hata sijui naenda wapi..huku akili yangu ikiamini kuwa nimeuwa tena mbaya zaidi nimeuwa mbele za watu mnacha kweupe...
hata ile safari yangu ya kuelekea studio kuifata simu yangu ikaishia hapohapo..baada ya kukimbia umbali usiopungua kilometa mbili(2) hivi"" nilipunguza mwendo na kuanza kutembea watu walikuwa wakinishangaa nilipokuwa nakimbia kwa sababu ilikuwa mchana..lakini mimi sikujali hilo...""
nikaamua kwenda kwa mjomba wangu anaeishi kirumba ni mbali kidogo ilinichukuwa kama lisaa limoja kufika kirumba kwa sababu nilikuwa natembea kwa miguu..ilikuwa kama mida ya sa tisa na dakika kadhaa za mchana.
hata mjomba wangu alishangaa sana kuniona kwa sababu sikuwa na mazoea ya kwenda kumtembelea""
karibu CHOTA...habari za miaka aliuliza mjomba "
safi tu Uncle za hapa kwenu?" nilijibu hivyo
********
natoka naenda kwenye kikao cha chama alisema mjomba""
si nitakukuta ama? aliuliza kho kho..nilikohoa nikajibu kwa kigugumizi ndindindioo uncle uuutanikuta
mjomba aliondoka..
daah sijui atakuwa amekufa na kama amekufa si nitaozea JELA? nilijisemea moyoni"" nilikaa kama masaa matatu hivi(3) lakini niliona humo ndani hapakaliki niliamua kuondoka na kuelekea kule nyumbani kwa rafiki yangu tunapoishi" wakati natoka nje ya geti katika jumba hilo la kifahari alilokuwa akiishi mjomba wangu niliona pete chini kwenye mchanga niliipenda pete ile"" ilinivutia sana kutokana na rangi zake zilizokuwa zinawaka waka utadhani ndani ya pete ile kuilikuwa na taa inayomulika! nilisita kuiokota pete ile, lakini lilikuja wazo la tamaa nikajisemea kimoyomoyo bila shaka hii pete kitani chake kitakuwa imetengenezwa kwa madini ya Almasi hivyo nitaiuza nitapata pesa...nikakumbuka filamu flani hivi niliyoangalia miaka miwili nyuma iliyopita" filamu hiyo ilikuwa inaitwa (blood Diamond) nikakumbuka ni jinsi gani watu walikuwa wakiuwawa na kugeukana kwa sababu ya Almasi nilitabasamu na kujipa imani kuwa kama hiyo pete itakuwa imetengenezwa kwa madini ya Almasi basi nitaiuza kwa pesa nyingi..hivyo nitapata pesa ya kufanya video ya wimbo wangu mpya nilioupa jina la (USIENDE) nilichuchumaa nakuiokota pete ile ..niliiangalia kwa umakini zaidi" kwa sababu sikuwahi kumiliki cheni/pete/saa zilizotengenezwa kwa Madini ilipelekea mimi kutojua chochote kuhusu madini...wakati bado nimechuchumaa nilitaka kuivaa pete ile lakini nikasita na kuiweka kwenye kimfuko kidogo kilichokuwa pembeni mwa begi langu nikafunga zipu nakuanza kutembe taratibu huku nikiwaza kuhusu Tukio nililolifanya Leo mchana
******
Yapata mida ya saa mbili(2) hivi usiku nikiwa njiani naeleke kule ninapoishi nikaona mkusanyiko wa watu wakiangalia Taarifa ya habari kwenye grosari(grocery) nikajiunganao kuangalia taharifa ya habari nilishtuka baada ya kusikia habari ya............
itaendelea.............
je ni taharifa ipi aliona CHOTA kwenye runinga??
Usikose kufatilia Riwaya za Yozz Piano Tz sehemu ya nne(4)
[1/16, 02:02] MAYA WA HADITHI🔴: Riwaya:PETE YA AJABU
Mtunzi: Yozz piano Maya
whatsapp: 0656292416
Sehemu ya nne(4)
nilishtuka baada ya kusikia taharifa ya habari! kwenye kituo cha habari kiitwacho channel ten katika runinga nilipojisogeza kutazama hapa grosary(grocery)""" mtangazaji alisikika akisoma hivi""
leo majira ya saa tisa(9) mchana Mmekutwa mtu kauwa na watu wasiojulikana na kutupwa ndani ya mfereji"""
sikutaka kuendelea kusikiliza taarifa hiyo nilihisi jasho jembamba likinitoka huki ikiambatana na vijambo visivyokuwa na nukta (bhu bhu buh) niliingiwa na hofu kubwa ambayo siwezi hata kuelezea""
nilihisi kila mtu aliyekuwa pale..ameniona na kujua kuwa mimi ndio niliyefanya tukio hilo...mbaya zaidi kunamtu alikuja kwa upande wa nyuma yangu na kusema mbona umesimama hapa nilistuka nikahisi ni polisi kumbe alikuwa muhudumu wa grosari(grocery) hiyo akimaanisha kwamba nikae kwenye kiti...
wakati bado natafakari nikajikuta nikipiga hatua taratibu kurudi nyuma.
ikasikika sauti ya mtangazaji ikitokea kwenye runinga hiyo hapo grosari(grocery) nilishusha pumzi ndefu baada ya kusikia jina la huyo mtu aliyekuwa kauwawa...lilitajwa kwa jina la Masawe Lymo
nikagundua kuwa hakuwa yule mtu niliye mpiga ngumi ya jicho na kumpiga teke kali tumboni akaangukia ndani ya mfereji...
sikutamani kuendelea kukaa sehemu ile nikaondoka zangu kuelekea nyumbani kwa rafiki yangu,ninapo naishi.
******
nilitembea umbali kama hatua mia tatu(300) hivi....nikafika
nilimkuta rafiki yangu alikuwa anaangalia tamthilia ya ISIDINGO
Dah yule jamaa aliyekuwa anakudai kaja hapa na polisi maneno hayo aliyasema rafiki yangu niliyekuwa napenda kumtania kwa jina la Chamdo
mmmh! kapajuaje hapa nilijiuliza enhe ikawaje? niliuliza kwa shauku ya kutaka kujua kilichojili
aah amedai kuwa alipwe shilingi elfu hamsini nimempa lakini utanirudishia pesa yangu ukipata alisema Chamdo huku akifungua mlango na kutoka nje..hapo nikapata imani na nikarudi katika haliyangu ya kawaida kutoka katika dimbwi la mawazo aaaah ninamkosi gani mimi nilisema kwa sauti....
******
nilitoa begi langu mgongoni na kulitupia kitandani....sikukumbuka kulitoa begi yangu nilipoingia ndani kutokana na uwoga/wasiwasi uliokuwa umenitawala.
nilifungua zipu ya kimfuko kidogo kilichokuwa pembeni mwa begi langu hilo dogo(lasket) nikaitoa ile pete niliivaa kwenye kidole cha katikati cha mkono wangu wa kulia aaaah nikaivua nikaivaa kwenye kidole cha mkono wa kushoto....nilitabasama nakuiangalia pete ile kwa kuzungushazungusha kiganja changu nzuri" nilisema kwa sauti
****
nilivua nguo zangu na kujifunga taulo kuelekea bafuni kwa ajili ya kujisafisha mwili(kuoga)
nilichukua kama dakika tano(5)nikawa nimemaliza koga nikarudi chumbani...amani ilinitawala sana sikujua hata amani hiyo ilitoka wapi...pia nilijihisi yu-mwenyenjaa nilifunua hot-port lililokuwa mezani nikamuita rafiki yangu ili aje tule kwa sababu ata yeye alikuwa akinisubiri tuje kula pamoja oyaaa Chamdo......chamdoooo aliitika
njoo tule nilisema kwa sauti kutokana yeye alikuwa nje mimi nilikuwa ndani...
aaah we endelea me nipo namalizia kufua si unajua kesho job sitopata muda mpaka weekend ijayo alisema Chamdo..
*****
nilikula baada ya kumaliza nilipanda kitandani nikawa natafuta usingizi....
kutokana na uchovu na mizunguko/kutembea umbali mrefu sikuchukua dakika nikasinzia nililala usingizi mzito naweza kusema ulikuwa usingizi wa ajabu""""
nikiwa usingizini niliona mambo mengi ya ajabu tena ya kutisha niliona watu wengi wakiwemo viongozi mashuhuri na watu maarufu hapa duniani kwenye jumba kubwa lililo enea vitu vya thamani wakati huo na mimi nikiwemo miongoni mwao""
niliendelea kuona mambo mengi ya kustahajabisha ambayo sikuwahi kuyaona zaidi ya kusimulliwa au kuyaona kwenye filamu....nilimuona Mzingu amekaa mbele yetu amevalia mavazi meupe kanzu refu lililofunika miguu yake isionekane alafu katikati ya vazi hilo kwenye kifua kulikuwa na picha niliitazama kwa umakini picha ile nikagundua kuwa ilikuwa picha ya FUVU la kichwa cha binadam...Mzee yule wa kizungu Alimuita mtu mmoja mmoja...
alifanya hivyo kwa wote tuliokuwemo mule ndani..
ilipofika zamu yangu nilifatwa na wanawake wawili wakiwa wavalia mavazi mekundu kuanzia kichwani mpaka chini kutokana na urefu wa mavazi waliyovaa sikuweza kuona miguu yao.......
walinichukuwa na kunipeleka pale mbele kwa yule mzungu kisha wakasujudu nilistahajabu sana kuona mtu kalala juu ya meza huku damu ikichuruzika(ikitiririka) kutoka kwenye shingo ya mtu huyo niliweza kutambua kwa haraka jinsia yake kwa sababu alikuwa uchi wa mnyama
alikuwa ni binti wa miaka kama 16 au 17 hivi......
niliogopa yule mzungu akaongea kwa rugha ya kiswahili usiogope alichukua kikombe chenye muonekano wa bati la njano linalong'aa sana (dhahabu) alikinga DAMU kwenye shingo ya binti yule . nakunipa huku akisema kunywa niliogopa nikastuka usingizini ..mapigo yangu ya moyo yalienda mbio huku jasho likinitoka...niliangalia kushoto kulia sikuona kitu nikawasha taa na kuitazama saa pale ukutani yapata saa9 tisa usiku...nikajipa moyo kuwa hii ni ndoto tuu..
nililala masaa machache pakakucha..niliamka na kwenda kuoga.. nilipofungua mlango wa bafuni nilipiga kelele baada ya kuona...................
Itaendelea.............
je CHOTA aliona nini bafuni??
ungana na Yozz Piano Tz kwa muendelezo wa Riwa hii yeny kusisimua sehemu ya TANO(5)
[1/16, 02:03] MAYA WA HADITHI🔴: Riwaya: PETE YA AJABU
mtunzi: Yozz Piano Maya
Whatsapp 0656292416
Sehemu ya tano(5)
Nilipiga kelele niliogopa sana niliina joka kubwa lenye rangi ya kijivu na macho yake yalikuwa na rangi nyekundu" lilikuwa limejiviringisha kwenye sakafu alafu limeinua kichwa juu(hewani) ...niliusukuma mlango wa bafuni kwa nguvu(puu) kwa lengo la kuufunga alafu nikasogea mbali kama hatua kumi hivi....wakati huo mwili wangu ulikuwa unatetemeka kwa uwoga...
nilipotaharuki nikajikuta nipo uchi yani taulo lilidondoka pasipo mimi kujua..nilichuchumaa kwa ajili ya kuficha nyeti zangu nikaangalia kushoto kulia sikuona dalili ya mtu yoyote aliyekuwa karibu...nikanyanyuka haraka nakupiga hatua za harakaharaka kulifata taulo langu pale chini ya mlango wa bafu lilipokuwa limedondoka""" nililiokota kwa staili ya kulivuta kwanguvu kama mwizi anapokwapua kitu kutoka kwenye mikono ya binadamu au mfano wa mwewe anapokwapua kifaranga cha kuku/bata chini ya Aridhi..
*****
nilijifunga taulo langu na baada ya kuhakikisha nimelifunga baraabara nilielekea upande wa pili wa nyumba kuufuata mti kwa lengo la kukata kipande kirefu cha mti yani fito" nilikata fito ndefu na kurudi kwa hatua za kunyatia..kama ninja au chui anavyonyata anapokuwa na njaa, baada ya kuona mnyama kwa mbali""""
niliendelea kunyata taratibu huku mapigo yangu ya moyo yakienda mbio ikiambatana na vijampo vya uwoga vya mfululizo .
(phu phu phu) nilipoukaribia mlango wa bafu nilisita kuufungua lakini nikaingiwa ujasili niliufungua kwanguvu( vuu) lakini cha stahajabisha sikuona kitu chochote nilibaki mdomo wazi nikafikicha macho yangu nikahisi labda bado nipo usingizini nilijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu....nilighahilisha kuoga nikarudi chumbani....nilipoigia nilisikia manukato yanayonikia vizuri sana....sikuwahi kusikia manukato yale tangu nizaliwe nilijiuliza Manukato haya nani kayaleta humu ndani na sikuona mtu aliyeingia..
mmh! nilkguna tu nikaendelea na mambo yangu...nilivaa nguo nkachukua viatu pia nikavaa miguuni mwangu nikazifunga kamba vizuri kabla ya kutoka Chamdo alirudi alikuwa ametoka kwenye mazoezi ya mpira...yeye huwa anaamka alfajiri na kwenda uwanjani kufanya mazoezi...sikumsimulia kilichotokea nikaondoka zangu kuelekea studio...
********
baada ya kufika studio nilifanya kile nachokifanya kila siku kuhusu muziki wangu.....
ikafika mida ya saa nane mchana nilijihisi njaa pia prodicer wangu akasema hata yeye anajihisi njaa tuliamua kuelekea kwenye mgahawa uliopo jirani na studio nakumbuka nilikuwa na shilingi elfu tano kwenye M-PESA nikaenda kwa wakala nikatoa shilingi elfu nne..wakati naweka mfukoni zile shilingi elfu nne nilishangaa kukuta pesa mfukoni nilipozitoa ili kuhakikisha kama ni pesa nilishangaa baada ya kuzihesabu zilikuwa noti za shilingi elfu kumi kumi mpya zilikuwa laki tatu..nilijiuliza pesa hizo zimetoka wapi? au ni za chamdo? itakuwa majisahau kaweka kwenye jinsi ya akidhani ni jinsi yake nilijisemea kimoyomoyo"""
sikutumia hata shilingi katika hizo pesa....
******
tulimaliza kula tukarudi studio
aaaaah wamekata tena umeme alisema producer....sikuona sababu ya kuendelea kukaa studio niliamua kuondoka zangu..
wakati nikiwa njiani natembea liliniijia wazo la kwenda bichi ( beach ) nilipofika bichi nilijilaza kwenye mchanga..kutokana na upepo mwanana uliovuma kutoka baharini na kupuliza nchi kavu nilipitiwa usingizi nikiwa usingizini nilimuona mwanamke mzuri sana mweupe mrefu na wenye nywele nzuri ndefu zenye muonekano mzuri aisee uzuri wake hakuna mfano....
yule mwanamke aliniita jina langu CHOTA alafu akasoge mpaka nilipo nikamuuliza umejuaje jina langu akatabasamu na kusema usijali....alijitambulisha kwa jina la marha ni kisha akanikumbatia nilistuka kutoka usingizini sikuona mtu yoyote...
yapata mida ya saa kumi na moja za jioni..
*****
nikanyanyuka na kujifuta mchanga nikaelekea kwenye guba. (maji ya bahari yanapoishia katikati ya bahari na nchi kavu) nilipotazama upande wangu wa kulia kwa mbali nilimuona manamke amekaa kenye meza yenye mwamvuli anakunywa juisi aisee nilistahajabu huyu si ndio yule mwanamke niliemuona usingizini??? nilijisemea moyoni nilichukulia kawaida nakusema kwa sauti ya chini aaaahhh! ndoto za mchana bhana noma kweli nikatabasamu...
nilichuchumaa na kuchota maji kwa kiganja changu nikanawa uso....
kutokana na ukubwa ka ile pete niliyoiokota na kuivaa kwenye kidole changu ilikuwa ikinipwaya kutokana na vidole vyangu kuwa vyembamba... pete ile ili iliponyoka kidoleni na kutumbuki kwenye maji ya bahari kwa sababu nilikuwa nimechchumaa kwenye jiwe niliamua kuvua viatu na kukunja jinsi (jeans) yangu ili niingie kwenye maji kwa lengo la kuiokota kutoka humo kwenyemaji""
kutokana na kina kile kifupi pete ile ilionekana vyema wakati nainama kuichukua lilikuja wimbi kubwa likapiga wimbi hilo lilipelekea nguozangu kulowana na pete ile sikuiona tena pale ilipokuwepo mara ya kwanza roho iliniuma sana.... mara nikaiona kwa mbali kwa sababu ilikuwa inang'aa sana....nikajisemea moyoni kwa sababu nimeshalowana potelea mbali ngoja niifate..nikapiga hatua kama hatua tatu hivi nikaikaribia...lakini wakati huo maji alikuwa yakiendelea kujaa taratibu kuja upande ule niliokuwepo kwa mbali nililiona wimbi kubwa lililokuwa linakuja kwa kasi ya ajabu likiambatana na upepo uliovuma kwa kasi na msauti ya mivumo...utadhani kuna mtu anapiga mluzi kwa mbali..nilipiga hatua mbili za haraka kwa lengo la kuifikia pete ile...wakati huo akili yangu iliwaza kamba wimbi lile la kwanza lilikuwa dogo lakini liliisogeza pete mbali tena kwakuisogeza kuelekea baharini je hili wimbi linalokuja??? wakati nikijiuliza hivyo"" niliona watu wengine waliokuwa wakicheza michezo mbalimbali ndani ya maji wanakimbia kutoka ndani ya bahari na kuelekea nchi kavu.
******
ghafla kurudisha macho kuangalia pale pete ilipokuwepo nilikuwa nimechelewa niliirukia aiseee niliruka kama goli kipa anayerukia mpira....kiasiambacho kama ningekuwa kipa basi hakuna mpira ambao ungepigwa golini nikashindwa kuudaka....nilifanikiwa kuishika pete ile kwa mkono wa kushoto nikaivaa haraka kwenye kidole ili isiniponyoke......wimbi lile kubwa lilinipiga (puu) na kunivuta ndani zaidi kuelekea baharini
sikujua kilichoendelea"" nilipopata fahamu nilijikuta nipo kwenye Jumba kubwa nimezungukwa na............
Itaendelea.......
Je? CHOTA alipozinduka alijikuta yuko wapi? na amezungukwa na nini/akina nani? usikose kufatilia muendelezo wa simulizi hii ya kusisimua sehemu ya sita ( 6)
ungana nami Yozz Piano Tz
[1/16, 02:04] MAYA WA HADITHI🔴: Riwaya: PETE YA AJABU
mtunzi: Yozz piano Maya
whatsapp:0656292416
Sehemu ya sita (6)
Nilipo zinduka nilijikuta nimo ndani ya jumba kubwa huku nikiwa nimezungukwa na watu wengi...watu hao niwale niliowaona kwenye ndoto" jana usiku......pia niliwaona viongozi mbalimbali wa dini.na viongozi wa nchi mbalimbali na wasanii maarufu... safari hii haikuwa ndoto tena bali ilikuwa ni kweli niliona kwa macho yangu mambo yale(live)
*****
pia nilimuona mjomba wangu yule anayeishi kirumba... nilistahajabu sana mmh! kwani mjomba anafanya nini hapa au yeye ndiye aliyenileta? nilijiuliza bila kupata jibu...
watu wote waliokuwemo mule ndani walikuwa wamesimama wima huku wameinamisha vichwa vyao chini....wakiwa wamevalia mavazi mfano wa kanzu jekundu hata lisioneshe miguu yao........mara punde akatokea mwanaume Mzee mwenye asili ya kizungu hata ukimuona kwa mbali inadhihirisha wazi kuwa ni mzungu" nilishangaa sana kumuona yule mzee wa kizungu aaah!!! huyu si ndiye yule mzee niliemuona kwenye ndoto jana usiku?? nilijiuliza huku nikikodoa macho yangu vyema, aisee ndio yeye..... na kwanini mambo haya yanatokea?? nilijiuliza bila kupata jibu.
****
nikanyanyuka kutoka pale chini nilipojikuta nimelala baada ya kupata fahamu..
nikasimama nilipogeuka nyuma ili niangaze angaze macho Kama kunamlango ambao upo wazi nikimbie nilistuka baada ya kugeuza shingo yangu nyuma..nilimuona yule mwanamke niliemuona usingizini kipindi nimelala kule bichi (beach) tena akiwa amevalia mavazi yale yale niliemuonanayo usingizini...alikuwa kavaa gauni la bluu (blue) refu tulipokutanisha macho alitabasamu..niligeuza shingo yangu haraka nikaangalia mbele kule alipokuwa amesimama yule mzee wa kizungu....watu wote walikaa chini kwenye kapeti wakapiga makofi mara tatu..alafu wakabaki hivyohivyo mfano wa mtu aliyeshikanisha mikono huku akiomba msamaha...niliendelea kuwatazama kwa makini watu wale niliona wakipishanisha vidole vyao sikuelewa walikuwa wanafanya ishara gani...
uwoga ulipungua kidogo na wasiwasi ukanitoka kwa sababu nilimuona mjomba wangu...lakini sikuwa na amani....
******
yule mzee wa kizungu alizipiga hatua na kuelekea upande niliokuwa nimesimama niliogopa sana...aliponikaribia alicheka sanana kwa sauti ya kutisha...akanyamaza ghafla na kusema wewe ni shujaa watu wenye nyota kama yako ndio tunawataka..... nilizidi kuogopa wasisiwasi ukatawala sana....nilihisi leo ndio siku yangu ya kufa nilisikitika sana kwa sababu jana niliona bintinti wa miaka 16 au 17 hivi amechinjwa nikapewa kikombe chenye damu ya binti yule kwamba ninye...niliikumbuka ndoto ile niliyoota jana usiku wa manane.....niliamini kwamba leo itakuwa zamu yangu...machozi yalinilenga na nilipopiga kope tone la chozi lilidondoka likatiririka kwenye shavu langu la upande wa kulia...yule mzee wa kizungu aliniambia usiogope kijana...nilimtazama kwa uwoga wa hali ya juu""
mapigo ya moyo yalienda mbio kwa kasi ya ajabu ikiambatana na vijampo vya mfululizo(phu phu phu) hiyo yote ilitokana na uwoga niliokuwanao..wakati wote huo sikuwa nikimuangalia yule mzee wa kizungu usoni.. sasa niliinua kichwa changu na kumtazama usoni niliona namba kwenye paji la uso wake namba hizo zilisomeka (666) yani triple six... sikuweza kutambua chochote kuhusu hizo namba zilizopo kwenye paji la uso la Mzee huyu wa kizungu!!
******
alizipiga hatua na kirudi kule mbele alipokuwa amesimama...
nilitazama ule upande aliokuwepo mjomba nilimuona mjomba kakaa lakini mikono yake kaiweka kwa nyuma sikuweza kutambua kwa haraka haraka kwamba alikuwa na maana gani kuweka mikono nyuma...
****
ilisikika sauti kutoka kule mbele, ilikuwa ni sauti ya yule mzee wa kizungu ikiita jina la mjomba...."
mjomba alisimama na kuzipiga hatua kuelekea kule mbele alipokuwa yule mzee wa kizungu...
wakati mjomba anazipiga hatua ndipo nikagundua kwa nini mjomba alikuwa ameweka mikono nyuma nilishtuka sana nikaingiwa na woga mara mbili zaidi baada ya kuona kamba zimefungwa kwenye mikono ya mjomba....
alipomkaribia yule mzungu alisimama kisha akasujudu.." duh!! kwani huyu mzee wa kizungu ni nani nilijiuliza...
ikasikika sauti ya yule mzee wa kizungu ikiuliza NGAO yako iko wapi?? nilikodoa macho huku masikio yangu yakiwa makjni kusikiliza kile ninachokisikia na macho yalikiwa makini kutazama kile ninachokiona... mjomba alijibu ewe" mfalme wangu pete yangu imepotea na sikumbuki nimeipoteza katika mazingira yapi kwa sababu jana nilipokuwa natoka nyumbani kwangu nilikuwa nayo ewe" mfalme wangu...
*******
umevunja mashart na kanuni zetu lazima utumikie adhabu na adhabu yenyewe ni kifo hakuna namna..alisema yule mzee wa kizungu.
*****
hapo ndipo nikagundua kuwa ile pete niliyookota pale nje ya geti la nyumba ya mjomba kumbe ndio pete hiyo inayozungumziwa hapo...nilitazama kidole changu kuiangalia ile pete nilipaza sauti PETE YAKO NINAYO hii hapa... nilizipiga hatua kutoka pale nilipokuwa nimesimama na kuelekea kule mbele walipokuwa wamesimama mjomba na yule mzee wa kizungu nilipoivua ile pete mjomba alianguka chini nakuanza kutoka moshi mdomoni niliogopa nikaivaa haraka pete ile mjomba akarudia hali yake ya kawaida..wakati naishangaa pete ile kidoleni kwangu ghafla nilisikia kishindo puuu......
itaendelea..........
usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua..
ungana nami Yozz piano Maya katika sehemu ya saba (7)
[1/16, 02:05] MAYA WA HADITHI🔴: Riwaya: PETE YA AJABU
mtunzi : Yozz piano Maya
whatsapp:0656292416
Sehemu ya saba(7)
nikasikia kishindo (puuu) kuangalia mbele niliona kiwiliwili cha mjomba wangu kimelala chini kikiwa hakina kichwa damu zilimwagika nyingi...
wakati huo wale watu wengine walikuwa wakiimba kwa sauti ya libesi zito hayskusikika maneno wanayoimba ilikuwa mfano wa mtu anayeguna mfululizo bila kupumzika. aisee niliogopa sana..kisha yule mzee akasema karibu katika familia mpya...
******
nilimuuliza kwanini umemchinja huyu mtu?? sikuweza kusema kuwa ni mjomba wangu niliogopa kusema hivyo kwa kuhofia kwamba wakigundua kama ni mjomba wangu watanichinja na mimi"
******
yule mzee wakizungu alinifata na kunishika kichwani aisee sikuamini kilichonitokea nilijihisi mwenye amani nikawa sina uwoga kabisa tena niliona kama nipo tu nyumbani sehemu yenye usalama kabisa....
*****
ale watu wengine waliondoka na sikuona walipoelekea nikachukulia kawaida sikufatilia sana....alikuja Marha na kunishika mkono...aliniongoza kuelekea upande wa juu....tulipanda gazi hatua kwa hatua kuelekea juu nilikuwa nikistahajabu jumba lile lilivyo kubwa na lenye korido na konakona nyingi...
tulifika katika mlango mmoja ulikuwa umeandikwa herufi tatu pale juu.... na herufi hizo zilisomeka (N.W.O) nilimuuliza marha hizi herufi zinamaana gani?? marha alitabasamu lakini hakujibu kitu chochote...alifumgua mlango huo tukaingia upande wa ndani...niliona kitanda kikubwa cha raundi(round) alafu chumba kilikuwa kikinukia manukato maruzi sana...aliniambia CHOTA utalala hapo kwenye kitanda hicho...
mmh! alafu wewe utalala wapi? nilimuuliza akacheka na kujibu kuwa nitalala hapohapo...
sikusema chochote alinipatia taulo na kuniongoza bafuni nilishindwa kuoga peke yangu baada ya kukumbuka matukio yale niliyoyashuhudia kwa macho yangu...
marha alinishika mkono akaingia na mimi bafuni...alivua nguo bila kuogopa chochote utadhani kwamba alikuwa anaoga peke yake...
aliniangalia kwa mahaba nikajikuta huku chini mzigo unasimama tena ulisimama wima baraabara.. kutokana na maungo yake yanavyovutia hasa sehemu ya kiuno na makalio meupe.
nilijizuia nikaendelea kuoga lakini yeye alikuwa wa kwanza kumaliza kuoga atangulia kutoka bafuni....
na mimi nikamaliza muda huo huo haikupita dakika... nikatoka bafuni..nilishangazwa sana na kitendo cha kumkuta marha ameshavaa na kutengeniza nywele na kujiremba pia kabadilisha nguo...hicho kilikuwa ni kama kitendo cha sekunde tano tu...nilibaki namuangalia kwa jinsi alivyopendeza hata nisikumbuke kuhusu chochote nilichokiona chumbani humo
******
baada ya kumaliza kuvaa nguo zangu..marha aliniambia unaonaje usiku wa leo twende club nilimkubalia pendekezo lake tukatoka mpaka nje ya jumba hilo kubwa...
*****
marha alifungua mlango wagari akapanda na mimi nikafungua malango wa kushoto nikaingia ndani ya gari...aliwasha gari na safari ya kuelekea club ikaanza baada ya umbali kama wa kilometa sita(6)tulikutana na beria matrafki wale walikuwa wazungu Marha alitoa kadi/kitambulisho akawaonesha wakaturuhusu kupita wakati marha amarudisha kadi/kitambulisho sikuona maandishi yoyote kwenye kadi ile zaidi ya namba zilizosomeka (666) yani triple six.. tulifika club.. marha alipaki gari tukashuka...
****
Nilistahajabu kuona taa nyingi zenye rangi ya kila aina zikiwaka nje ya club ile nilipoangalia kwenye lango la kuingia ndani ya club hiyo niliona bango limeandikwa( wolf loyar club) tulipoingia ndani waafrika tulikuwa waxhache yani hata watano hatufiki wengi wao walikuwa wazungu..sikutaka kucheza muziki wala sikunywa chochote kwa sababu kila niliemuona alikwa amesika glasi yenye DAMU ndani yake.. ilipo fika mida ya saa tisa na dakika moja( 9:01) za usiku wa manane mziki ulizima ghafla na watu wote waliokuwako mule ndani ya club walitoweka ghafla sikuona mtu hata mmoja hata marha pia sikumuona..
nilipotoka nje sikuona hata lile gari tulilokujanalo
nilistkuka nikaogopa sana...nilipogeuka nyuma nilistahajabu tena niliingiwa na hofu na uwoga waa hali ya juu baada ya kuona club ile haikuwepo tena pale ilipokuwa mwanzo nilikimbia lakini sikuona nyumba waskuona mtu yoyote yule niliamua kusimama mara ghafla nikavutwa sikuona aliyanivuta lakini nilijikuta nimo chumbani..kwenye kile chumba tulichokuwepo na Marha safari hii nilimuona marha akiwakatika sura nyingine ya kutisha na meno marefu pia alikuwa na kucha ndefu...niliogopa nikajifunika uso wamgu kwa viganja vya mikono yangu ghafla marha alirudia hali yake ya kawaida..........aisee safari hii nilimuogopa sikutamani hata kumkaribia...
alinitazama kisha akasema usiogope tulikuwa tunamuabudu ILUMINATI...
iluminati??? iluminati ndio nani?? nilimuuliza akatabasamu na kujibu ILUMINATI ni MUNGU WETU...
sikuendelea kuhoji lolote. alinitoa hofu na wasiwasi tukalala.
*********
nilipostuka asubuhi nilijikuta nimelala makabulini kwenye makaburi ya kinondoni juu ya kaburi moja hivi....nilishangazwa kuona jina la Marha kwenye kaburi lile alafu pembeni kulikuwa na picha ya marha nilipoiangalia niligundua ni marha..nikaigeuza kwa nyuma nikakuta anuwani za....
Itaendeleaaaaaa..............
usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua
ungana nami Yozz piano Maya kwenye sehemu ya nane (8)

Maoni 2 :

  1. Mimi ni Black Rambo kutoka Grammy, ninafanya kazi katika Kambi ya Grammy, mke wangu alifariki mwaka 6 iliyopita na tangu nimekuwa nikimtunza mwanangu pekee aitwaye Clinton, rafiki yangu wa ushauri wangu wa kumtafuta mke, kwenye upekuzi wangu nilikutana na Jennifer alikuwa na mwanamke wa Kiingereza, Nilimpenda sana kiasi kwamba ningeweza kumpa kila kitu alichokuwa na umri wa miaka 37, baada ya muda fulani wa uchumba nilikuwa na mapenzi sana naye, tulikuwa na kutokuelewana, na alivunja na mimi na ninamsihi arudi mwanangu aitwaye alisema Hapana, kwamba amempata mtu mwingine, na tunapendana sana baada ya siku kadhaa nilisoma makala kuhusu jinsi Dk Lomin anaweza kusaidiana , Niliamua kutoa jaribu, nawasiliana na Dk Lomi kwa msaada aliniambia nini cha kufanya ili kumrudisha mpenzi wangu niliyefanya, alifanya maombi na Jennifer alikuwa nyuma ananipenda na kunithamini zaidi sasa, na tuna wakati mzuri wa maisha yetu, Dk Lomi pia kuandaa baadhi ya mimea ya asili ambayo imenifanya niwe na nguvu na afya tena sasa nahisi kama kijana niliyemridhisha vizuri sana sisi sote tuna furaha, wasiliana na Dk Lomi kwenye WhatsApp namba +2349034287285 au barua pepe yake kwenye lomiultimatetemple@gmail.com ANA SULUHISHO BORA KWAKO.

    JibuFuta
  2. CHUMA ULETE YA CHUNGU

    Kwanza CHUMA ulete Ni nini?
    Ni dawa ambayo utengenezwa kwa mkusanyiko wa utaratibu Fulani unaofanyika kwa pamoja kwa mlengo wa uvutaji au uvunaji wa fedha kutoka sehemu tofauti au mbalimbali.

    (Kwa uhitaji wa NDAGU AU JIHNI WA MALI AU FEDHA NA KINGA YA MWILI NA MALI KWA UJUMLA NIPIGIE SIMU MOJA KWA MOJA DOKTA MDIRO +255 742162843 KWA MAELEKEZO HATA KAMA UKIWA MBALI MALIPO NI BAADA YA MAFANIKIO).

    CHUMA ulete katika utengenezwaji hutumika jini anayeitwa GHUUL ambae uleta au uvuta fedha kimazingala kutoka sehemu mbalimbali kwa utaratibu maalumu. CHUMA ulete zipo Aina nyingi Ila leo nitazungumzia CHUMA ulete mdogo ya CHUNGU.

    Chuma uleteee ndogo ya chungu ambayoo inaluka na kwenda kukusanya pesa sehemu mbali mbali inavuta pesa ndanii .

    Hii chakula chake ni udi tuu na unaweza kunuwiza ukachagua ukaomba ikuletee pesa za aina gani wewe utachaguwa kama unavyoona hapo kwenye picha hii ni chuma uleteee ndogo mtu yeyotee anaweza kutengenezewa hata kama huna biashala pia hata Kama upo mbali kikubwa tu uwe na uwezo wa kutunza sili. Vile vileee hii inadumu miaka 5 itakubidii uludi kuja kutengeneza upya kafara ya damu ya kuku mwekunduu inatakiwa kila baada ya miezi 3.

    Tafuta chungu kama icho kwenye picha fanya duwa maalumu ambayo nitakupatia na tafuta udi Aina ya sain frola, metrofrolla au metromillan na kitambaa cheupe pia chumba kisafi kwa ajili ya ibada hiyo.

    Kumbuka hii ni chuma uleteee ndogo ya chungu hutakiwi kutoaa sili ya jini huyu na ufalume wa jini huyu maana utavunja miiko na maagano ya Jambo Hilo.

    Angalizo Piga simu kuepuka MATAPELI pia kwa maelekezo zaidi husifanye jambo hili bila maelekezo KAMILI.

    DOKTA MDIRO

    Call/whatsup +255 742162843

    JibuFuta