JINA: kazi yangu
MTUNZI: Davis Nyandindi
NO. 0679962818
MTUNZI: Davis Nyandindi
NO. 0679962818
SEHEMU YA 3

REHEMA: Kama alivyo tangulia kusema mchungaji hapa, ni kweli mm ninaitwa rehema na ninatokea sumbawanga. Ninajua wengi sana mliniona jinsi nilivyo kuwa ile siku ya jumapili na mliniogopa sana, ila kwa upande wangu ile hali ndio maishangu ya kila siku na ndio ilikuwa KAZI YANGU. Kiukweli nimekuwa nikiifanya ile kazi kwa mda mrefu sana tangu nina zaliwa mpaka sasa hizi nimetiza juzi miaka ishirini na mbili nikiwa kwenye ile kazi. Ila tangu nianze ile kazi mpaka sasa hivi, sijawai kuona faida yake hata siku moja, zaidi ya adhabu na mateso ya muovu shetani kila siku. Maana kutokana na ile kazi nilizuiriwa nisisome, wala kuolewa au kuwa na mchumba, na kila nilipokuwa nikijifanya mbishi kuwa na mchumba, mara moja huyo mwanaume alikua akipotea kimazingira ya kutatanisha sana au kupoteza maisha kabisa, hali iliyopelekea mimi kuachana kabisa na mambo ya mahusiano tangu siku hiyo. Mara kwa mara nilikuwa nikijaribu kujitoa katika ile shughuli lakini nilikuwa ninashindwa, na wale wakuu wa ile kazi walikuwa wakiniambia kuwa endapo nitafanikiwa kujiondoa nitakufa, maana mimi ni mtu wao ambae nilipekwa tangu nikiwa mchanga na kulelewa na wao.
Rehema baada ya kusema vile tu, yule mchungaji akachukua kipaza sauti kingine na kuanza kumuuliza maswali kutokana na kile ambacho alikuwa amekionge.
MCHUNGAJI: Rehema umesema wale wakuu wa ile kazi walikuambia kuwa wewe ni wao maana ulipelekwa kwao wakati upo mtoto mchanga na wakakulea wao mpaka umekuwa binti mkubwa hivyo,. Sasa je waliwai kukuambia kuwa ni nani ambae alikupeleka kwao wakati upo mchanga?.
REHEMA: ndio waliwai kuniambia.
MCHUNGAJI: Je waliwai kukuambia sababu ya kukupeka uko?.
REHEMA: Ndio waliwai kuniambia.
MCHUNGAJI: Vizuri, basi ninaomba utuambie ni nani alikupeleka huko na alikupeka kwa sababu gani, maana ninataka watu wa MUNGU wajue jinsi gani shetani pamoja na mawakala zake wanavyo fanya kazi.
Basi yule mchungaji baada ya kusema vile, akazima kile kipaza sauti chake na kumuachia nafasi Rehema ili andelee kutoa ushuhuda pamoja na majibu ya yale maswali ambayo alikuwa amemuuliza.
REHEMA: Kwa maelezo yao waliniambia kuwa mama yangu mzazi ndie alinipeleka mimi kwao. Na kisa cha yeye kunipeleka huko alitaka sichezewe na wachawi, maana katika mtaa ambao tulikuwa tukiishi kipindi hiko, mara kwa mara watoto wa changa walikuwa wakifariki kila wanapo fikisha wiki moja tangu wazaliwe.
Rehema baada ya kusema vile, yule mchungaji alimstopisha kuongea na kuanza kumuuliza maswali mengine.
MCHUNGAJI: Kwahiyo mama yako wakati anakupeleka huko, alikuwa ajui kuwa alikuwa anakupeleka sehemu mbaya kiasi kile, au yeye alijua anakupeleka sehemu salama ?.
Yule mchungaji baada ya kuuliza vile alinyamaza na kumuachia rehema nafasi ya kujibu.
REHEMA: Hapana kwa mujibu wa maelezo ya wale wakuu, mama yangu alikuwa hajui kama alikuwa ananipeleka sehemu mbaya kiasi kile. Maana waliniambia baada ya kufikusha siku tatu tangu nizaliwe, mama alinichua na kunipeleka kwa mganga ili anifanyie dawa ya kunikinga na wachawi, majini, na mashetani, na alikula kiapo fulani kule kwa mganga, na hiko kiapo ndio kilichofanya mimi niwe wao tangu siku ile, na zile dawa ambazo nilipewa huko kwa mganga ndio ikawa kama alama yangu na njia ya wachawi kunipata kwa urahisi, ila vyote hivyo mama yangu alikuwa hajui kitu chochote kile.
Basi rehema baada ya kusema vile, yule mchungaji akadakia tena na kuongea maneno fulani na kuwasihi waumini wake kuto amini mila na desturi za kishirikina.
MCHUNGAJI: Jamani Wapendwa si mmesikia hii, na kila siku nimekuwa nikiliongelea jambo hili kuwa msipende kuwapeleka watoto wenu kwa waganga wa kienyeji, maana huku mnaenda kuwa sababishia matatizo mengi sana. Mara kwa mara mmekuwa mkilalamika kuwa watoto hawaelewi mara hawana akili wakiwa mashule, kumbe mambo yote hayo mnasababisha nyie wenye wazazi alafu mwisho wa siku mnakuja mlaumu MUNGU kuwa hakuwapa mtoto mwema kumbe ni ujinga wenu nyie wenyewe. Sasa leo nina rudia tena kusema hivi, endapo MUNGU wetu mwema akikujaria kupata mtoto, moja kwa moja mlete hapa kanisani, tutamuombea na wala hakuna kibaya chochote ambacho kitamkuta, maana huyu tunae muabudu hapa leo ni MUNGU alie hai na mwenye uwezo na nguvu kuliko kitu chochote hapa duniani na hata uko mbinguni.
Basi yule mchungaji baada ya kusema vile, watu walipiga makofi pamoja na vigeregere, na baada ya hapo mchungaji akamruhusu rehema aendelee kutoa ule ushuhuda.
REHEMA: Basi baada ya mama kunipeleka kwa mganga, tulirudi nyumbani huku akijua kuwa nimepata kinga na nitakuwa salama na sitakufa kama ilivyokuwa kipndi cha nyuma. Sasa kwa maelezo ya wale wakuu waliniambia kuwa baada ya kutimiza wiki moja tu, ndipo nilianza kazi rasmi, na kazi yangu mimi ilikuwa ni kuuwa watoto wachanga wenzangu kwa kuwanyonya damu zao. Niliambiwa kuwa kila mtoto ambae alikuwa akitimiza wiki moja au mbili, mimi ilikuwa inatumwa nafsi yangu, na kwenda kuuvaa mwili wa huyo mtoto, yani kama jini na baada ya hapo ndio ninaanza kumnyonya damu yake na baada ya siku kadhaa tu yule mtoto anapoteza maisha ghafra, au anapandikiziwa ugonjwa fulani, ili aonekane kuwa amefariki kwa ugonjwa huo. Ila watoto ambao tulikuwa tukiwafanyia hivyo, ni wale ambao wazazi wao walikuwa awamtumainii huyu MUNGU tunae muabudu hapa, bali wao kila kitu chao walikuwa wakifanya kwa njia yao wenyewe pasipo kumshirikisha MUNGU WAO.
SEHEMU YA 4
KUPATA MUENDELEZO WA SIMULIZI HII JIUNGE NA KUND LINAITWA #SIMULIZI ZA DAVIS NYANDINDI LIPO FACEBOOK
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni