JINA: kazi yangu
MTUNZI: Davis Nyandindi
NO. 0679962818
SEHEMU YA 4
MTUNZI: Davis Nyandindi
NO. 0679962818
SEHEMU YA 4

Rehema baada ya kusema vile, yule mchungaji akamnyamazisha na kuanza kuongea yeye.
MCHUNGAJI: Jamani nyie wamama na wababa ninahisi mmesikia hii sasa kazi kwenu, kuacha watoto wenu wachukuliwe na shetani au kuwa kabidhi mbele za MUNGU ili mkae nao kwa mda mrefu ili mwisho wa siku mvune mema kutoka kwa watoto wenu.
Yule mchungaji baada ya kusema vile, akanyamaza na kumuachia nafasi rehema ili aendelee na ushuhuda wake.
REHEMA: Basi niliendelea kufanya hivyo mpaka nilipotimiza miaka mitano, ndipo kazi ya kunyonya damu na kuuwa watoto wa watu ndipo nikasitishwa na kupewa mtoto mwingine. Sasa baada ya kusitishwa ile kazi, nilichukuliwa na kupelekwa sehemu ambayo kwa kipindi hiko sikujua ni sehemu gani lakini ilikuwa ni chini kabisa ya ardhi. Na kila mtu ambae tulikutana nae huko alikuwa akitisha sana, maana hakuna ambae alikuwa mweupe au kuonekana sura yake, bali wote walikuwa weusi kupindukia utadhani mtu ambae alikuwa amekaa kwenye moshi tangu kuzaliwa kwake mpaka pale alipofikia. Basi baada ya kufika huko, tulipokelewa na hao watu na baada ya hapo tulipelekwa sehemu fulani, ambayo sehemu hiyo tulikutana na mtu ambae alikuwa amekaa kwenye kiti kikubwa chenye rangi nyeusi na alikuwa tofauti kabisa na wale wenzake, kuanzia sula mpaka kila kitu chake, maana sura yake ilikuwa haionekani bali ikionekana kama kivuli cha kichwa chenye pembe mbili, na pili hatuku ruhusiwa kusegea karibu na huyo mtu. Basi baada ya kukaa kama hatua ishirini au kumi na tano mbali na yule mtu, wale wazee pamoja na wale watu wa ajabu tulio wakuta kule, wote walimsujudia yule mtu na kuniacha mimi nikiwa nimesimama peke yangu, na baada ya hapo wote wale waliongea maneno fulani kwa pamoja, ambayo mimi kwa kipindi hiko sikuelewa nini walikuwa wana maanisha. Basi wale watu baada ya kufanya vile, yule mtu alijibu kwa maneno ambayo sikuyaelewa, lakini sauti yake ilikuwa ya juu sana na yakutisha sana, ambayo endapo kama huyo mtu angekuja hapa na kuonge japo neno moja tu, nina amini kama hauna nguvu za MUNGU lazima ukimbie, maana inatisha kupita kiasi. Basi yule mtu baada ya kujibu ile salamu, mzee mmoja ambae tulifuata nae sisi, aliinua kichwa chake na kuanza kuongea na yule mtu kwa kutumia lugha yetu ya kiswahili, na yule mzee aliongea hivi.
MZEE: Mkuu yule mtoto tulie kuahidi kukuletea ndio huyu hapa mbele yako, kwahiyo tunaomba nguvu zako na umpatie huyu mtoto ili aianze kazi yako sasa, maana sasa hivi bado hana nguvu yoyote ile, kwahiyo hataweza kuifanya kazi yako.
Basi rehema baada kunukuu yale maneno ya yule mzee akaendelea kusimulia nini kiliendelea baada ya yule mzee kusema vile.
REHEMA: Basi yule mzee baada ya kusema vile, ghafra yule mtu akaanza kucheka kwa sauti kubwa sana ambayo ilimtetemesha kila mmoja watu na kila kitu kilichopo kule chini tulikuwa tumeenda. Sasa baad ya yule mtu kucheka kwa sauti kubwa vile, ghafra nililikuja giza nene nene nene yani hata siwezi kuelezea hilo giza jinsi lilivyo maana tangu nizaliwe mpaka hivi leo sijai ona giza nene kiasi kile hapa duniani. Basi baada ya kuja hilo giza, zilipita sekunde kadhaa, lile giza likawa limetoweka na baada ya lile giza kutoka tu, ghafra nilijikuta nikiwa nimefungwa kaniki huku nikiwa nimeveshwa hilizi saba, na hilizi nne zilikuwa nyeusi na tatu zilikuwa nyekundu, na hizo hilizi zenyewe ninataka leo zichomwe moto hapa mbele ya watu wote ili tumuaibishe shetani pamoja na kazi zake zote.
Basi rehema baada ya kusema vile, waumini walishangilia kupita kiasi na baada ya kumaliza kushangilia, kabla Rehema hajaanza kuongea yule mchungaji akadakia tena na kuaanza kumuuliza mwaswali.
MCHUNGAJI: Ehe rehema unaweza kutumia hizo kaniki na hizo ilizi zilitokea wapi, Pia unaweza kutuambia hizo kaniki pamoja na hizo hilizi zilikuwa zinakazi gani?.
REHEMA: Kiukweli mpaka leo hii sifahamu vile vitu vilitokea wapi, maana sikuwai kuambiwa jambo hilo kuhusiana na upatikanaji wa zile nguo. Ila kuhusu kazi ya vile vitu niliambiwa na vyote nitawaeleza kazi zake.
MCHUNGAJI: Sawa mwanangu tuambie kazi za vile vitu.
Basi yule mchungaji baada ya kusema vile, ndipo rehema akaanza kueleza kazi ya zile hilizi pamoja na ile kaniki.
REHEMA: Kwanza ngoja nianze na ile kaniki, ile kaniki ilikuwa ni kama vazi la kazi, na nilikuwa siruhusiwi kufanya kazi yoyote bila ya kuivaa ile kaniki, maana ilikuwa ikiniongezea nguvu fulani. Ila zile hilizi kila moja ilikuwa na kazi tofauti na yenzake, na zile ndio zilikuwa tegemezi kubwa sana kwangu.
SEHEMU YA 5
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni