Jumapili, 22 Januari 2017

KAZI YANGU SEHEMU YA (5)

JINA: kazi yangu
MTUNZI: Davis Nyandindi
NO. 0679962818
SEHEMU YA 5
Picha ya Davis Nyandindi
REHEMA: Kwanza zile hilizi kila moja ina ukubwa tofauti na yenzake na jinsi ilivyo kuwa tofaut kiumbo basi na kazi ilikuwa hivyo hivyo, na ndogo kuliko zote ilikuwa nyeusi. Hiyo ilizi ndogo kuliko yote kazi yake ilikuwa kama ufunguo pindi ninapotaka kuingia sehemu yoyote, na ufunguo huo uko tofauti kabisa na hizi mnazozijua nyie ambazo tunafunguliaga milango, funguo hiyo ilikuwa inafungua ukuta maana wachawi wengi milango yao huwa ni ukuta, maana baadhi milango ya nyumba watu uwa wanawekaga vitu vyao ambavyo mda mwingine utuzuia sisi kuingia ndani. Kwahiyo hilizi ndogo ndio ilikuwa ikifanya kazi ya kufungua njia ya sisi kuingilia ndani. Hilizi ya pili kwa udogo ilikuwa ni nyekundu na kazi ya hilizi hiyo ilikuwa ikitoa taarifa ya hatari ya sehemu tuendako, na hiyo taarifa ilikuwa ikijionyesha kwa ile hilizi kuwaka na kuzimika kwa rangi nyekundu huku ikiwa inatoa mlio kama wa mluzi. Ile hilizi pindi ikifanya hivyo, tulikuwa tukijua kuwa huko tuendako kuna hatari kwahiyo inatubidi kufanya mambo mawili, kwanza kujipanga na kujiongezea nguvu au kugailisha hiyo safari, ili tusipate hasara ya kualibika vitu vyetu. Hilizi ya tatu ilikuwa ni nyeusi na kazi ya hilizi hiyo ilikuwa ni kuniongezea nguvu pale ninapo onekana kuzidiwa na nguvu zingine tofauti na zile nilizonazo mimi.
Rehema baada ya kusema vile, yule mchungaji akamnyamazisha na kumuuliza swali fulani ambalo lilikuwa na faida kubwa sana kwa waumini wake.
MCHUNGAJI: Ehe rehema umesema hiyo hilizi ya 3 kazi yake ilikuwa ni kukupa nguvu pale inapoonekana umezidiwa na nguvu nyingine, sasa je mbona ulishindwa kutoka pale ulipokuwa umenasa siku ile au hiyo hilizi haukuwa nayo mda ule?.
REHEMA: Hapana ile hilizi nilikuwa nayo, lakini nguvu za MUNGU nilizo kutana nazo pale zilikuwa ni kubwa kuliko nguvu zangu na nguvu ya ile hilizi na ndo maana nikashindwa kutoka.
Rehema baada ya kusema vile, waumini walishangilia Sana na baada ya hapo yule mchungaji na yeye akaongezea maneno yake ili kuzid kuwatia iman wale waumin.
MCHUNGAJI: Wapendwa si mnasikia na mimi kila siku ninawaambia kuwa hakuna kitu wa mtu yeyote ambae anaweza kuishinda kuvu ya huyu MUNGU wetu, na ndio maana ukimtumainia yeye tu lazima mambo yako yaende sawa na wala hakuna atakae izuia baraka yako.
Basi yule mchungaji baada ya kusema vile, rehema akaendelea kueleza kazi ya zile hilizi nne zilizokuwa zimebakia.
REHEMA: Hilizi ya nne ambayo ilikuwa nyekundu, kazi yake ilikuwa kuniwezesha kubadilika kutoka kwenye sura yangu kwenya sura ya mtu wowote yule,. Hilizi ya tano ilikuwa ikinisaidia nisionekae ninapokuwa kwenye kundi la watu na ilikuwa ikinisaidia kwenye shughuli zangu za chuma ulete. Hilizi ya sita nilikuwa nikitumia kwa kuwasiliana na wenzangu pale ambapo ninakuwa niko mbali nao kikazi, na hilizi ya sita ambayo ni kubwa kuliko zote, ilikuwa ikinisadia kutoka katika umbile la kibinaadamu na kwenda umbile la mnyama wowote yule au ndege, pia hilizi hiyo ilikuwa na kazi ya kuzisadia zile hilizi zingine zote.
Basi baada ya kuelezea kazi za zile hilizi, rehema akaendelea kusimulia nini kilitokea baada ya kupewa vile vitu na yule mtu ambae sura yake ilikuwa ni kivuli tupu.
REHEMA: Basi baada ya kubadilika na kuwa nimevaa ile kaniki, wele wazee walifurahi sana kwa kupiga makofi pamoja na vigeregere maana tulikuwa tumefuatana na wamama kama watatu hivi. Basi baada ya hapo wale wazee walimuaga yule mtu na ghafra tukapotea pale ambapo tulikuwa tumepiga magoti na kutokea kwenye kambi yetu ambayo ilikuwa katikati ya mbuyu mmoja mkubwa sana ambao ulikuwa upo katikati ya mji. Tulipofika huko tuliwakuta wenzetu wengine wakiwa wanaimba na kucheza kwa kufurahia kutokana na ile hatua mbayo mimi nilikuwa nimeifikia, kwa hali ya kawaida jambo lile nililo fanyiwa mimi ninaweza kuita ni kama unyago. Kiukweli nilifurahi sana kuona vile maana, kipindi hiko nilikuwa bado sijaona madhara ya ile kazi na japokuwa nilikuwa ni mdogo lakini nilikuwa nikiipenda kupita kiasi ile kazi yangu. Basi baada ya mda kadhaa kupita, mkuu wa ile kambi alitunyamazisha na kuanza kuongea maneno ya kunikribisha rasmi kwenye maisha ya kiutuuzima kwa upande wa kiuchawi, ninanukuu maneno ya yule mzee.
MZEE: Rehema karibu sana kwenye ulimwengu mpya na kuanzia sasa hivi wewe sio mtoto tena kama unavyo jiona, bali sasa hivi wewe ni mtu mzima na una uwezo wa kufanya kitu chochote kile.
REHEMA: Yule mzee baada ya kusema vile wenzangu walifurahi sana, na ndipo yule mzee akaniambia kuwa kwa kuwa nimeshakuwa mtu mzima ninatakiwa ile siku mimi ndio nipeleke nyama ya kula watu wote pale. Basi yule mzee baada ya kusema vile mimi nilimchagua mama yangu mdogo ndie tumfanye nyama sikuile na kwa bahati mbaya kipindi hiko huyo mama yangu alikuwa ni mjamzito na siku zake za kujifungua zilikuwa zimekaribia sana kwahiyo alikuwa amelazwa hospital. Basi baada ya kumchagua huyo mama yangu, tulitoka watu kama kumi mpaka kwenye hodi ya wamama wajawazito ambayo mama yangu mdogo ndio alikuwepo umo. Sasa baada ya kufika humo, tuliwatia upofu watu wengine wote lakini kwa wale ambao walikuwa wakimwamini mungu tulishindwa fanya hivyo.
rehema baada ya kusema vile, yule mchungaji akamnyamazisha na kumuuliza swali kuhusiana na kile ambacho alikuwa amekiongea.
MCHUNGAJI: Ehe rehema umesema mliwatia watu upofu lakini wale wanao mwamini MUNGU mlishindwa fanya hivyo, sasa je wao hawakuwaona wakati mnafanya kazi yenu.
REHEMA: Hapana walikuwa hawatuoni lakini nguvu ya MUNGU iliwashukia na wote wakawa wakiomba ili wasipatwe na baya lolote kutoka kwetu, pia mda wote walikuwa wakizungukwa na nuru.
MCHUNGAJI: Sawa, endelea.
Basi yule mchungaji baada ya kusema vile rehema akaendelea na kusimulia.
SEHEMU YA 6

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni