Jumanne, 31 Januari 2017

KENGERE YA KIFO SEHEMU YA NNE(04).

Riwaya: KENGERE YA KIFO
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CONTACT: 0656292416
Picha ya Yozz Piano Maya Tz
SEHEMU YA NNE(04)
***ilipoishia***
pembeni kulikuwa na gari jingine limesimama..ndani ya gari hilo kulikuwa na familia alikuwemo Mwanamke Mtoto pamoja na baba wa mtoto ambaye aliyekuwa akiliendesha gari hilo....kulikuwa na vitu vingi vya kuchezea mtoto wao ndani ua gari hilo ghafla yule mtoto akachukua kengere ya kuchezea watoto.......mtoto hiyo aliitingisha kengere ile kwa kuigonga gonga kwenye kiti cha gari....ghafla Tina akasikia mlio wa kengere hiyo.....akastuka.....
***Endelea***
Domy alitoa simu yake aina ya SAMSUNG NOTE 4
akampiga picha Tina...kitendo cha mwanga wa flash kuwaka kikazuia hali ya tina kubadilika...ghafla taa za alama za barabarani zikaruhusu magari yaliyokuwa uoande wa kushoto kuendelea na safari...kabla hawajafika mbali tina akasema,," turudi nyumbani najisikia nafuu...Domy hakutaka kumpinga Tina...akakatisha kona na kuingia kwenye barabara nyingine...akiiacha ile barabara iliyokuwa ikielekea hospitali....Domy aliendelea kuzipanga gia huku akiliendesha gari lake kwa mwendo wa wastani.....
wakiwa njiani Tina akasema,,"Tupitie kariakoo kuna duka fulani hivi nikaangalie kama wameshaleta mapazia mapya....Domy akajibu,,"Sawa mke wangu kilenzi kisha akaliendesha gari mpaka kariakoo.....kutokana na msongamano wa magari kuwa mengi..Domy aliamua kulipaki gari kwenye hotel moja....ili Tina asguke aende dukani kwa sababu hapakuwa na umbali.......
wakati huo huo alionekana muhudumu wa hotel kwa upande wa jikoni akifunika chakula na kuzipiga hatua huku amekibeba chakula hicho kuelekea kwenye ngazi ya umeme(Lift) akaingia upande wa ndani mlango ukajifunga,,akabonyeza kitufe kilichoandikwa namba (6) lift ikaanza kupanda kuelekea juu....alipofika ghorofa namba sita akazipiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba (113) akabofya kengere iliyokuwa pembeni ya mlango huo..
****************
kule upande wa nje alionekana tina akizipiga hatua kuelrekea dukani..mara ghafla akastuka...akasita kuendelea kutembea akasimama...akaanza kubadilika macho yake yakaanza kutoa machozi...ghafla akatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere.....akajitokeza kwenye ile hotel juu ghorofa ya sita.....akazioiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba(113) alipofika akaingia upande wa ndani kimiujiza.....akamnyonga yule muhudumu pamoja na Mwanaume aliyekuja Hotelini humo kupumzika na mpenzi wake....baada ya Tina kufanya mauwaji hayo akatoweka kimiujiza na kujitokeza pale alipokuwa amesimama....Tina alionekana kujishangaa sana.....akahairisha kwenda dukani akazioiga hatua za harakaharaka kurudi kule lilipokuwepo gari la Domy...
wakati huohuo kabla Tina hajafika...alionekana Domy akiongea na simu,,ghafla salio likakakata akifungua mlango wa gari na kutoka upande wa nje ...akazipiga hatua kuelekea madukani kununua vocha....
baada ya Domy kutoka Tina akafika akafungua mlango haraka na kuingia ndani ya gari.....akabaki humo akimsubiri Domy...
**************
Upande mwingine kule kwenye Mgahawa wa Mzee Sule walionekana wateja wakiingia na kutoka huku upande wa nje yakionekana magari mengi na Bodaboda zimepaki nje ya mgahawa huo......watu walifurahia supu iliyokuwa inapikwa kwenye mgahawa huo.....pamoja na ugali nyama choma...mishkaki ,,soseji na sambusa...kwa mbali alionekana mteja mmoja akinyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi na kumfuata mke wa Mzee sule......mtu huyo alifoka huku akisema....,,"yani tangu nimefika hamjaja kunisikiliza!!!haya nataka ugali nyama choma...nichomee uenye mafutamafuta kiasi usikaushe sana...weka pilipili nyingi....kisha akarudi kuketi pale alipokuwa ameketi mwanzo...
*****************
Upande mwingine alionekana Mzee Sule....akitika nje ya nyumba yake iliyokuwa katikati ya pori kubwa huku amebeba matulubai matatu yaliyotengenezwa kama gunia,,akayarusha upande nyuma ya gari lake..akaingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake......
wakati huhuo kule lilipokuwa limepaki gari la Domy, alionekana Tina kujishangaa huku akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu!!!!!!
kwa mbali alionekana Domy akizioiga hatua kuja pale lilipokuwepo gari lake huku akiongea na simu..alipofika alifungua mlango na kuingia ndani ya gari....akaendelea kuongea na simu hiyi kwa dakika kadhaa,,alipomaliza akambusu Tina shavuni huku akisema,,"samahani mke wangu,, nilikwenda kununua vocha. Tina alibaki kimya akatabasamu...Domy akaliwasha gari wakaondoka kuelekea nyumbani....
walipotoka tu wakapishana na gari la Mzee Sule.likiingia ndani ya hoteli hiyo...Tina akastuka akamtazama kwa mshangao Mzee Sule...huku akijiuliza moyoni,"Mbona kama namfananisha huyu Mzee!!!sijui nishamuona wapi????Tina akabaki na mshangao kichwani mwake...huku Domy akiendelea kuzipanga gia kuelekea nyumbani.......
*****************
alionekana Mzee Sule akishuka kutika ndani ya gari lake na kuelekea ndani kabisa ya Hotel hiyo....akaimgia ndani ya ngazi ya umeme(lift)akabofya kitufe kilichoandikwa namba(6) alipofika ghorofa ya sita akazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba namba(113)huku ameshikilia ile mifuko mitatu mikubwa iliyotengenezwa kwa kutumia tulubai......akafungua mlango na kuingia upande wa nadani.....
baada ya Mzee sule kuingia ndani ya chumba hicho kwa mabali alionekana kijana mmoja akizipiga hatua za harakaharaka kumfuata Mzee Sule.....kumbe kijana huyo ni muhudumu wa Usafi upande wa vyumbani....akanyata mpaka mlangoni akachungulia upande wa ndani kwa kupitia tundu la ufunguo.....akastuka hofu ikamjaa alipogeuka ili akimbie mara ghafla......ikasikika sauti......
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya Tano(05)
pia usisahau ku-Like page yangu inayoitwa
MAYA WA HADITHI .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
like pia share na marafiki.
ASANTENI....‎

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni