Ijumaa, 27 Januari 2017

KENGELE YA KIFO. SEHEMU YA KWANZA(01)



Riwaya: KENGELE YA KIFO
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CINTACT: 0656292416
DAR ES SALAAM.
SEHEMU YA KWANZA(01)
Ilisikika taarifa ya habari katika kituo cha habari hapa nchi. taarifa hiyo ilielezea kuhusu binti mmoja aliyezikwa miaka 50 hiliyopita...binti huyo alifufuka na kuanza kuonekana sehemu mbalimbali huku macho yake yakionekana kuwa na machozi ya damu iliyoganda...inasemekana kuwa binti huyo anajitokeza kila unaposikika mlio wa kengere yoyote ile.....anabadilika sura na kufuata mlio wa kengere ulipotokea,,na akifika eneo hilo anafanya mauwaji ya kikatiri kwa kunyonga shongo kwa kutumia kamba aliyokuwa anatembeanayo muda wote.kila anapobadilika....hakuna aliyekuwa akifahamu kuwa binti huyo alifufuka na anaishi katika maisha ya binadamu wa kawaida,lakini huwa anabadilika na nacho yake hutoa machozi ya damu kila inaposikika sauti ya kengere...
Usiku wa leo,binti huyo aitwae Tina..alionekana akiwa ndani ya clubu akiwa na mpenzi wake Domy....walikuwa wameketi kaunta huku wakinywa
karinya(pombe)Domy alikuwa hajui kuwa Tina alishakufa miaka hamsini (50)iliyopita akazikwa huko,Nigeria lakini alifufuka Tanzania..Domy aliishi na Tina miaka mitano lakini hakuwahi kuwajua wazazi wala ndugu wa tina..pia hakuwahi kumjua rafiki wa tina hata mmoja..hata simu ya tina ilikuwa na namba moja tu ya Domy.
waliendelea kunywa pombe...Tina akanyanyuka ili aende chooni kujisaidia haja ndogo..alipoingia chooni ikasikika kwa mbali sauti ya kengere ikitokea upande wa nje ya club..uso wa Tina ukaanza kubadilika macho yake yaanza kutoa machozi ya damu....akatoweka kimiujiza na kuelekea kule ulipotokea mlio wa kengere....
akajitokeza nje ya nyumba moja akaanza kuzipiga hatua..
kwa mbali kidogo walionekana wanafamilia wakiwa wamesimama mlangoni wakisubiri mlango ufunguliwe...walipo ona kijakazi wa ndani anachelewa kufungua mlango baba wa familia hiyo akabofya tena kitufe cha kengere ili yule kijakazi kama amelala basi aisikie kengere hiyo...
wakastuka kunamwanamke kasimama nyuma yao
akamkamata baba wa familia hiyo na kumnyonga kwa kamba aliyokuwa ameishikilia mpaka akafa.
mkewe akaamua kutimua mbio huku amewashika mikono watoto wake wawili wa kike... tina akajitokeza mbele yao na kuwanyonga wakafa papohapo...kisha akaingia uoande wa ndani na kumuuwa kijakazi wa nyumba hiyo....akatoka upande wa nje na kutoweka kimiujiza.....akajitokeza ndani ya choo cha cha wanawake ndani ya ile club aliyomuacha Domy...akarudi katika hali yake ya kawaida akatoka chooni na kurudi kule kaunta.. wakaendelea kuzitandika karinya(kunywa pombe)
ilipofika majira ya saa saba za usiku Domy alisema waondoke wakalale....wakatoka nje na kuingia ndani ya gari wakaianza safari ya kurudi nyumbani...
*****************
asubuhi palipokucha alidamka na kuandaa chai..
alipomaliza kuandaa chai wakaanza kunywa huku wakitaza Runinga...ikaoneshwa taarifa ya habari ikisema kunafamilia imeuwa na mtu asiyejulikana.
kisha wakainesha ile nyumba ya wanafamilia hao.
Tina alichukia akakaza macho kuitazama runinga ghafla ikavunjika kioo.. na kuanza kutoa moshi...
Domy alistuka sana lakini hakujua kuwa Tina ndiye kavunja Runinga hiyo kimiujiza..Domy akaanza kulalamika kwa kusem,,"Yani hili shirika la tanesco hawapo makini na kazi yao,ona sasa Runinga yangu imeeungua....Domy alikasirika sana akahairisha kunywa chai akaondoka na kuelekea kazini....kabla hajafika mbali aliamua kwenda nyumbani kwa rafiki yake...hakuna umbali mrefu kutoka nyumbani kwake...alipofika alipaki gari na kuufuata mlango akagonga hodi..akasubiri kwa sekunde kadhaa alipo ona hakuna mtu anayekuja kufungua mlango,,akahisi huenda hawajasikia akigonga mlango akaamua kubofya kengere iliyokuwepo kando ya mlango kwenye ukuta.
****************
Kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akiendela kufanya usafi wa nyumba...ghafla ukasikika mlio wa kengere akili ya tina ikabadilika pamoja na uso wake...macho yake yakaanza kutoa mchozi ya damu...akatuoa kitambaa alichokuwa anakitumia kuduta vumbi kwenye kabati la sebuleni......akatoweka kimiujiza na kuufuata mlio wa kengere..........
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya pili(02)
 .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
like pia share na marafiki.
ASANTENI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni