Ijumaa, 3 Februari 2017

KENGERE YA KIFO SEHEMU YA SABA(07)

Riwaya: KENGERE YA KIFO
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CONTACT: 0656292416
SEHEMU YA SABA(07)
Picha ya Yozz Piano Maya Tz
***ilipoishia***
Tina alishindwa kujibu kutokana yeye hafahamu chochote....haijui siri nzito iliyopandikizwa mwilini mwake......
wakati huohuo walionekana wale walevi wakigonga geti kwa nguvu....ye mle mmojawapo akabonyeza kengere kwa mara nyingine tena.
Domy akiwa anamuuliza Tina maswali mara ghafla Tina akastuka....akainamisha uso wake chini......Domy alikasirika sana aliona kama Tina kamdharau kuwa yeye anamuongelesha alafu Tina kainamisha uso wake chini....
Domy akaamua kumsogelea Tina huku amenyanyua mkono ampige kofi......
***Endelea***
Tina alipoinua uso wake, Domy alishtuka macho yakamtoka alistaajabu kumuona tina amebadilika huku macho yake yanayotokwa na machozi ya damu,Domy akatimua mbio kuelekea chumbani wakati huo huo wale walevi waliendea kubofya kitufe cha kengele,Tina akatoweka kimiuzija kuufuata mlio wa kengere.
****************
wakati huohuo ule upande mwingine walionekana wale walevi wawili..kisha mmojawapo akazipiga hatua kadhaa akasimama kando na kuanza kujisaidia haja ndogo...ghafa akajitokeTina akiwa kwa mbali kidogo kutoka hapo walipo walevi hao.....akazipiga hatua kuwafuata.....yule mlevi aliyekuwa akijisaidia haja ndogo akamuona Mwanamke akija upande wao huku ameinamisha uso wake chini.....yule mlevi akaingiwa Tamaa ya kutaka kumtongoza Tina...akafunga zipu haraka haraka.akasimama huku anayumba yumba kwa ulevi...Tina alipomkaribia yule mlevi akamfuata..ghafla Tina akainua uso wake...ye mlevi akastuka akaogopa sana Tina akamkamata na kunyonga kwa kutumia ile kamba yake....wakati huohuo yule mlevi mwingine akageuka akaogopa sana kumuona mwenzake ananyongwa....pombe zikamruka,,akaanza kutimua mbio..alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea..Tina akajitokeza mbele yake...akamkamata akamnyonga kwa kutumia ile kamba.......kisha akazipiga hatua kadhaa akatoweka kimiujiza.....baada ya sekunde kadhaa akajitikeza nyumbani..akawa anajishangaa..
********************
wakati huohuo Domy alionekana akiwa kajifungia chumbani huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu...jasho lilimtoka mfululizo...akaona chumbani hapakaliki,,akaamua kufungua mlango wa chumbani akachungulia kule upande wa sebuleni..akamuina Tina yupo katika hali yake ya kawaida huku akionekana kujishangaa....Domy akatoka chumbani huku akizipiga hatua za tahadhari..alitembea huku macho yake yakimtazama Tina...alipomkaribia akamuita Tina kwa sauti ya chini,,Tina...Tinaaaa
Tina akastuka akamtazama Domy...hali yake ya ufahamu ikarudi akaitika," Abee mume wangu.
Domy hakutaka kuuliza kitu chochote akaogopa hata kumsogelea.....Tina alijisikia vibaya,,alitamani kujua ni nini kimetokea lakini alishindwa jinsi ya kumuuliza Domy....Tina akaamua kuzipiga hatua kuelekea chumbani...akamuacha Domy kasimama palepale sebuleni,,Domy akajiuliza,,"yawezekana Tina ni jini...au niliona vibaya...mmh!! lakini sidhani kama macho yangu yalinidanganya....
***************
Upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee Sule.....alionekana yule mtu aliyeafiza ugali nyama choma akiendelea kula ugali pamoja na nyama hiyo matata....akapaza sauti,,"niletee chumvi na ndimu....pia niongezee pilipili..aliyasema maneno hayo huku akiendelea kutafuna minofu ya nyama......baada ya sekunde kadhaa kupita aliletewa vitu alivyoagiza...akachukua ndimu akakamulia kwenye nyama ile..kisha akaweka na pilipili..akachukua mnofu mwingine akala pamoja na tinge la ugali....ghala kunakipande cha nyama(mnofu) aliuona kama haujaiva vizuri ulikuwa haujakauka...akastuka akakitazama kwa makini akaona mchoro....akajisemea moyoni,,"mmh!!! mbona kama inaonekana ni tatoo! ng'ombe gani huyu alichorwa mchoro wa tatuu ambayo huchorwa kwenye mwili wa binadamu??
kutokana nyama ile ilikuwa imeshachomwa alafu imekatwakawa vipande...mchoro ule haukuonekana wote..ulionekana nusu tena kwa mbali sana...mtu yule akajipa moyo kuwa hiyo ni nyama ya ng'ombe..hakuwa na shaka kuwa kwenye mgahawa huo awawezi kupika nyama ya binadamu.......akajisemea moyoni,,"yawezekana mmiliki wa mgahawa huu ni mfugaji...itakuwa anang'ombe nyingi sana.....hata hivyo wanachoma nyama vizuri tamu sana..ndio maana watu wanajazana kula kwenye mgahawa huu usiku na mchana..
wakati huohuo alionekana mzee sule akiwa barani anaendesha gari lake...akakatisha kona na kutokezea kwenye ile nyumba ambayo wale walevi wawili walinyongwa na Tina..akachukua maiti zao na kuzirusha nyuma ya gari...kisha akaingia ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake.....
******************
Upande mwingine alionekana Domy akizipiga hatua za taratibu kuelekea chumbani...lakini alikuwa na hofu na wasiwasi kuhusu Tina huenda akamdhuru....akafungua mlango na kuingia chumbani akamkuta Tina amevua nguo kabaki mtupu(uchi) kajilaza kitandani......pia Domy akapanda kitandani,,kutokana na umbile la Tina kuwa na mvuto wa aina yake Domy akapata hamasa ya kuanza kumpapasa Tina.....akasahau yale yote aliyotoka kuyaona muda mchache uliopita.....Tina hakutambua wala kujua chochote kilichotokea kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kujitambua na kujizuia anaposikia mlio wa kengere.......
***************
upande mwingine walionekana maaskari wakiwa katika gari la polisi wakifanya doria kwenye mitaa usiku huo.wakakatisha kona na kuliegesha gari lao kando ya barabara kisha wakashuka kutoka ndani ya gari wakasimama barabarani kuhakikisha kila gari inayopita lazima ikaguliwe.....kumbe kunatukio la ujambazi limefanyika muda mchache uliopita ala majambazi wakakimbia na kuondika enei la tukio wakiwa na gari aina ya TOYOTA PICK UP.
wakati huohuo alionekana mzee sule akikatisha kona kuifuata barabara hiyo ambayo wale maaskari walikuwepo...aliliendesha gari lake bila wasiwasi akaingia kabisa kwenye barabara...
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya nane(08)
pia usisahau ku-Like page yangu inayoitwa
MAYA WA HADITHI .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
like pia share na marafiki.
ASANTENI....‎

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni