Ijumaa, 27 Januari 2017

SIKU YANGU. SEHEMU YA KWANZA(01)

Riwaya: SIKU YANGU
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CONTACT: 0656292416
DAR ES SALAAM
SEHEMU YA KWANZA(01)
Ilisikika sauti ya mwanamke akilia kwa sauti kali sana ndani ya sekunde chache.....kisha sauti hiyo ikatulia kimya....baada ya sekunde kumi ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia.....baada ya dakika kumi kupita,,zikasikika sauti zikisikika zikisema"sukuma kwa nguvu....usibane mapaja utamuuwa mtoto...ghafla ikasikika sauti ikisema ""mama weee...
baada ya sekunde tatu hivi ikasikika sauti tena ya mtotochanga akilia....mwanamke huyo aitwae Rose alijifungua watoto mapacha wote wa kiume.walipishana dakika kumi za kuzaliwa...Ross alifurahi sana..Akamshukuru Mungu kwa kujifungua salama...baada ya masaa mawili kupita alikuja mumewe aitwae SEBA....alifurahi sana akasema,nitakupa zawadi mke wangu..nakuahidi nitakununulia gari...Rose alifurahi sana kusikia kauli hiyo ya mumewe..
***************
kesho yake majira ya saa nne za asubuhi.. madaktari walimruhusu Rose kwenda nyumbani..kutokana Rose alikuwa na nyonga pana sana hivyo haikuwa vigumu yeye kuzaa.. alijifungua salama bila kufanyiwa upasuaji wala kuongezewa njia kwa kuchanwa ukeni.
Seba alimchukua mkewe pamoja na mama mkwe wake wakatoka nje ya hospital,,waliingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea nyumbani.
*************
ilipofika majira ya saa saba za usiku....mama yake na Rose aliamka....akanyanyuka kutoka kitandani akafungua begi lake na akatoa kaniki nyeusi akajifunga rubega...kisha akatoa mkoba mdogo uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya Nyumbu..
akaufungua na kutoa irizi mbili zilizokuwa zimefungwa kamba nyeusi nyemba....akazivaa irizi hizo.....akazipiga hatua mpaka kwenye kona ya chumba akasimama wima. huku makalio kayageuzia ukitani......akatoweka kichawi....akajitokeza ndani ya chumba cha mwanae.....Rose alikuwa kalala fofofo pamoja na mumewe Seba...Mama huyo aitwae Bi'CHENDA
akavua irizi moja yenye rangi nyekundu..akaitemea mate kisha akazipiga hatua kukifuata kitanda...alipofika karibu sana...akaanza kukizunguka kitanda mara tatu..kisha akamgusa pacha mmjoja kichwani kwa kutumia irizi hiyo...
akazioiga hatua na kueleke kwenye kona ya chumba hicho akageuka na makalio yakageukia ukutani kisha akatoweka kichawi.....akajitokeza chimbani kwake..akarudisha zile irizi kwenye kile kimkoba kilichotengenezwa kwa ngozi ya nyumbu..akavua ile kaniki nyeusi na kuirudisha ndani ya begi lake,,, akapanda kitandani na kujifunika shuka tayari kwa kuutafuta usingizi.. ghafla kulwa akaanza kulia kwa sauti kali...na doto akaanza kulia ..ghafla doto alinyamaza akatulia tuli...kama amelala.....kulwa aliendelea kulia kwa mfululizo mpaka Seba na Rose wakaamka...Rose alimbembeleza kulwa lakini aliendelea kulia mfululizo..akaamua kumnyonyesha lakini aliendelea kulia bila kunyamaza....rose alifanya jitihada za kumbembeleza ili anyamaze asije akamuamsha doto....hatimae kulwa akanyamaza..na baada ya dakika kadhaa kupita kulwa alisinzia kabisa....wakati huo Rose na Seba hawakujua kuwa doto tayari ameshachukuliwa kichawi na bibi yake...na kitandani kuna kipande cha mgomba wa ndizi na si mtoto..
*****************
asubuhi palipokucha Mama Rose alidamka mapema akafua nepi za mapacha hao ambao ni wajukuu zake..kisha akachemsha maji kwa ajili ua kumkanda Rose sehemu zake za siri....baada ya dakika kadhaa Seba alidamka akajianda na kwenda kazini aliamua kujiwekea maji ya kuoga pamoja na kunyoosha nguo zake kwa sababu alimuhurumia mkewe kwa kuwa ametoka kujifungua juzi....baada ya seba kutoka,, Rose naye alidamka akanyanyuka kutoka kitandani akaelekea chooni....aliponyanyuka tu kulwa akaamka akaanza kulia akamchukua na kumnyonyesha...alipomaliza kumnyonyesha,akambadilisha nepi...baada ya lisaa limoja kupita alistahajabu mpaka muda huo doto hajaamka..akaamua kumtikisa ili aamke..lakini doto hakuamka alipomgeuza akaona mikono na miguu ya doto imekakamaa..rose akapaza sauti,,"MAMAAAA njoo haraka..
upande wa nje alionekana Bi'Chenda amestuka kusikia sauti ya Rose....akajisemea moyoni,,"Tayari kumeshakucha..akazipiga hatua kuingia chumbani kwake akachukua ule mkoba mdogo akatoa kichuoa kidogo kilichokuwa na unga wa mfupa wa ALBINO uliochomwa na kusagwa ukawa unga .ili akampake doto asionekane kuwa ni kipande cha mgomba..kipindi watu watakapokuja msibani..akazipiga hatua kuelekea chumbani kwa Rose...
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya pili(2)
 .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
l
ASANTENI

Maoni 1 :