Jumatano, 18 Januari 2017

Riwaya: KITABU
Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
CONTACT: 0656292416
SEHEMU YA SITA(06)Picha ya Yozz Piano Maya Tz
***ilipoishia***
latifa aliamua kurudi akafungua mlango na kuingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake akafungua kabati na kukitoa kitabu cha chary....akakiweka ndani ya mkoba wake..lakini alisita akakitoa ili asome tukio linalofuta kwenye sehemu ya tano..akafunua kurasa haraka haraka mpaka sehemu ya tano kisha akaanza kusoma.......ghafla mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio...macho yalimtoka akaingiwa na uwoga wa hali ya juu akatimua mbio na kutoka nje huku akikiacha kitabu juu ya kitanda chake...
***Endelea***
latifa alitimua mbio huku anapiga simu kule kazini kwake....simu ilipokelewa. latifa akasema"Kimbieni tokeni hapo mtakufa muda si mrefu....
yile mtu aliyepokea simu hiyo alistahajabu akauliza ""latifa umepatwa na nini?? mbona sikuelewi???
""jamani nasema hivi ondokeni hapo haraka mtakufa wote..
mtu yule alikata simu ya latifa akaendelea na shughuri zake....lakini akili yake ilikiwa ikitafakari maneno ya Latiffa..akajisemea moyoni"au latifa kachanganyikiwa!!! aliamua kunyanyuka na kuwafuata watangazaji wenzake akaanza kueleza kile alichoambiwa na Latiffa wafanyakazi wenzake walipuuza wakaanza kucheka...mmoja akaropoka ""kwani nini ni wageni kwa Latiffa huwa anapenda sana utani...yele mtu aliyeeleza taarifa hiyo akaamua kuondoka akaingia kwenye ngazi ya kutumia umeme(lift) na kubonyeza kitufe ili lift ishuke upande wa chini...alipofika chini kabisa alitoka kwenye lift na kuondoka zake.....
kumbe latifa aliposoma kile kitabu cha chery kilionesha jengo kubwa lililokuwa na kuituo cha radio ghorofa ya tano....jengo lile lilifanan na mchoro wa kwenye hadithi ya kitabu cha chery...hadithi ilieleza kuwa kuna kiumbe wa ajabu alivamia jengo hilo na kuuwa watangazaji wote isipo kuwa watangazaji wawili...mtangazaji wakiume na mtangazaji wa kike.....
**************
yule mtu aliyeshuka kutoka kwenye lift kabla hajafika mbali alisikia vioo vikipasuka alipogeuka nyuma aliona vioo vya madirisha ya ghorofa ya tano ndivyo vinavyopasuka kisha akaona watu wanatupwa nje kupitia madirisha hayo....watu hao walidondoka chini na kupasuka vichwa.....mtu yule alikimbia haraka kuelekea kwenye tukio....alipofika aliogopa kuona watangazaji wenzake wote wameuwawa na kupasuka vichwa vyao....watu walikusanyika kushuhudia tukio hilo lakini haikufahamika ni nani aliyefanya tukio hilo.....
************
upande mwingine kule juu ya ghorofaya tano..alionekana yule kiumbe akiwa bado yumo ndani ya kituo hicho cha radio..akaharibu mitambo yote inayohusika kurusha mawimbi ya radio hewani..kisha akatoweka kimiujiza.....
muda mchache polisi walifika eneo la tukio..wakaelekea juu kwenye kituo hicho cha radio...waliweka siraha zao tayari kwa kupambana kisha wakaingia mpaka ndani ya kituo hicho(UCCTV)...walistahakabu kukuta kila kitu kimeharibiwa isipokuwa kamera za ulinzi zilizokuwa zimetegeshwa ndani ya kituo hicho...
polisi mmoja aliifuata kompyuta iliyokuwa inahusika kurekodi mambo yanayoendelea ndani ya kituo hicho......alipotazama matukio yaliyorekodiwa masaa machache yaliyopita..matukio yote yalionekana isipokuwa tangu kiumbe yule alipojitokeza kamera hazikuwa na uwezo wa kurekodi tukio lolote......kipande hicho kilionesha giza..... na baada ya kumaliza kufanya mauwaji pamoja na uharibifu wa vitu vilivyokuwemo humo ndaani..akatoweka na kamera zikaendelea kurekodi kama kawaida hakuonekama muuwaji katika kamera hizo..
yule askari alistahajabu sana akajisemea moyoni""
bila shaka kunajambo lilitokea ambalo sio la kawaida...kisha wakapiga picha kwa ajili ya upelelezi wakaondoka zao..
************
upande mwingine alionekana yule mtangazaji alinusurika kifo...akizipiga hatua za haraka haraka bila kujua ni wapi anakoelekea.....akachukua simu yake na kumpigia Latiffa....
latiffa aliipokea simu hiyo haraka""mtu yule akasema ""umejuaje kuhusu hili jambo kama litatokea???
latifa alidakia na kusema""jamani nakusihi waambie watu wote mtoke humo mdani mkimbiesipofanya hivyo mtakufa....
yule mtu alijibu""muda mchache uliopita wafanyakazi wenzetu wote wameuwawa na kutupwa kutoka ghofani mpaka chini.....kabla hajamaliza kuongea latifa alikata simu......macho ualimtoka jasho likaanza kumtiririka huku ikiambatana na vijampo vya uwoga(bhu bhu)
akatimua mbio kurudi ndani kwake akafunua kitabu cha chery akaendelea kusoma sehemu ya tano ili aone tukio linalofuata........latifa alistahajabu kuona tukio la mauwaji ya kutisha katika shule ya watoto(chekechea) aliogopa sana alipoutazama mchoro uliokuwa umechorwa kwenye hadithi ya kitabu cha chery sehemu ya 5
hakuelewa mchoro ule ulikuwa unafanana na sehemu gani alijaribu kuvuta kumbukumbu huenda alishawahi kuona shule hiyo....Latifa alistuka akazipiga hatua kurudi nyuma kwa uwoga huku amebaki mdomo wazi.......
ITAENDELEA.......
Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua
ungana nami YOZZ PIANO MAYA katika sehemu ya saba(07)
pia usisahau ku-Like page yangu inayoitwa
MAYA WA HADITHI .ili kupata mtiririko mzuri wa RIWAYA zangu kuanzia sehemu ya kwanza..
like pia share na marafiki.
ASANTENI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni